Nafasi Ya Matangazo

January 18, 2019

Mbunge wa Jimbo la Busega (CCM) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Dkt. Raphael Chegeni amepongeza uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta ya mawasiliano kwa kununua mtambo wa kudhibiti mawasiliano.
Chegeni ameyasema hayo leo baada ya  Rais Dk. John Magufuli kuukabidhi mtambo huo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa usimamizi.
“Kwakweli huu ni uwekezaji mkubwa sana kama serikali itaweka usimamizi mzuri, kwakuwa mimi ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji nitahakikisha nashiriki vizuri katika usimamizi wa uwekezaji huu,”amesema Dkt. Chegeni
Mapela leo Rais Dkt. John Magufuli alitembelea miundombinu ya mfumo wa kuratibu na kusimamia mawasiliano yote ya simu (Tele-Traffic Management System – TTMS) na kushuhudia makabidhiano ya mfumo huo kutoka kampuni za ukandarasi za Societe Generale de Surveillance S.A (SGS)na Global Voice Group S.A (GVG), na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge Job  Ndugai, Mawaziri, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, viongozi wa siasa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mfumo huo umewekwa kwa malengo ya kupata takwimu za mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi, kuhakiki mapato yote ya watoa huduma za mawasiliano nchini, kupata takwimu zinazohusiana na matumizi ya huduma za mawasiliano (simu za sauti, data na ujumbe mfupi), kugundua mawasiliano ya simu za ulaghai na kutambua takwimu za ada za miamala ya fedha mtandaoni.

Malengo mengine ni kusimamia ufanisi wa ubora wa huduma, kutambua taarifa za laini za simu, kubaini na kufungia simu zenye namba tambulishi zilizonakiliwa na kuwasilisha kwa Serikali mapato yanayotokana na mawasiliano ya simu za kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini.

Posted by MROKI On Friday, January 18, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo