Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2018

MTU mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ahamad Salum mkazi wa Kata ya Namiyonga Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ameuawa na Mke wake Sofia Swaleh  Kwa Kuchomwa Kisu Kifuani kutokana na Majibizano ya Kupika Chakula Kingine. Anaandika Joseph Mpangala-Mtwara

Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa kabla ya Mauaji hayo kulitokea Ugomvi baina ya Marehem na Mkewe ambapo Marehem alipikiwa Chakula na baada ya Kula Hakushiba hivyo akashinikiza Mke wake kumuandalia Chakula kingine Ndipo Ndipo Ugomvi ukaibuka na Ndipo Mke wa Marehem Sofia Swalehe akachukua Kisu na Kumchoma eneo la Kifuani na kupelekea Ahamad Salum kufariki dunia kutokana na kupoteza Damu Nyingi.

Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Mmoja ni Jirani Mussa Bakari ambaye aliingia ndani ya Nyumba baada ya kusikia Ugomvi ukiendelea na akashirikiana na Mke wa Marehem Sofia Swalehe kuua.

Aidha Kamanda Mkondya amewataka wananchii kutumia Viongozi wa Kiserikali na Kidini kuweza kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika Jamii.

'Nitoe rai kwa wananchii Magomvi hayana tija wajaribu kukaa na Kususuluhisha sio mnakaa na kugombana kwa kitu Kidogo mpaka mnapoteza Maisha kwa kitu Kidogo kama Chakula"
Posted by MROKI On Wednesday, May 23, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo