Wasamaria wema wakiwa wamewabeba watoto waliogongwa na gari la mizigo katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, eneo la Kituo Kipya, Gongo la Mboto, Dar es Salaam leo.
Na Richard Mwaikenda, GOMS
WATOTO wawili wamegongwa na gari la mizigo katika ajali iliyotokea mchana wa leo katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Ulongoni, Gongo la Mboto (Goms), Dar es Salaam.
Watoto hao wawili ndugu wa kike na wa kiume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka minne na mitano walipatwa na mkasa huo muda mfupi baada ya mama yao kuwaacha pembezoni mwa barabara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema ajali hiyo ilitokea wakati gari gari namba T 324 PTM lililokuwa kwenye mwendo kasi kuikwepa bodaboda iliyokuwa iliyokatiza ghafla mbele yake, ndipo likapoteza mwelekeo na kuwagonga watoto hao.
Gari hilo ambalo dereva alikimbia baada ya ajali kuogopa kipigo, liliwagonga watoto hao na kuingia kwenye mtaro, lakini kama siyo mtaro lingeingia kwenye nyumba na kusababisha maafa zaidi.Mwendesha bodaboda naye alikimbia kuogopa kipigo.
Watu wengine wakiwemo waendesha bodaboda wanaoegesha kusubiri abiria katika kona hiyo ilipo transfoma, walinusurika kwani wengi wao hawakuwepo na baadhi yao walikimbia baada kuliona gari hilo limekosa mwelekeo.
Wanasema kuwa mama mzazi wa watoto hao ambaye hakuwa mbali sana na eneo la ajali aposikia mkasa huo hakuamini na kilichofuata aliishiwa nguvu na kuanguka chini.
Baadhi ya wasamaria wema waliharakisha kuwachukua watoto hao waliokuwa kwenye hali mbaya na kuwaingiza kwenye Bajaji tayari kuwakimbiza hospitali kwa matibabu.
Ajabu iliyotokea ni kwamba baadhi ya waendesha Bajaji walikataa katakata kuwapeleka watoto hao Hospitali.
Watoto waliojeruhiwa wakiwa chini baada ya kuwaokoa chini ya gari kwenye mtaro
Watoto majeruhi wakiingwa kwenye moja ya bajaji kuwawahisha hospitali, lakini hata hivyo mwendesha bajaji hiyo alikataa kuwapeleka na kuwaamuru wawashushe. Source: Kamanda wa Matukio Blog
Wakihamia kwenye moja ya Bajaji kuomba msaada huo
Wakiwaingiza kwenye Bajaji ambayo walikubaliwa
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akilia kwa uchungu baada ya kuwaona watoto hao
Wakiangalia ajali hiyo
Gari hilo nusura liingie kwenye maduka yaliyopo eneo hilo, kilichozuia ni mtaro wa maji taka,
Trafiki akiangalia ajali hiyo
Breakdown ikiandaliwa kulivuta gari. Hata hivyo lilishindwa
Gari hilo likivutwa na gari la taka
0 comments:
Post a Comment