Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo inadhamini Kilimanjaro Marathon, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Gr
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon Moshi.
*************************
Wadhamini
wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa wito kwa watanzania na
washiriki wengine kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili kushiriki
katika mbio za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na
kuwavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
Rai
hii inakuja takriban wiki mbili kabla kufanyikakwa mbio hizo maarufu
ndani na nje ya nchi ambazo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000
kutoka nchi zaidi ya 45 mjini Moshi ambapo mbhio hizi hufanyika.
Akizungumza
jinini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
Pamela Kikuli, ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu, alisema tayari
usajili umeshafunguliwa na kuwataka washiriki hususan wale wa mbio za
kilometa 42 zinazodhaminiwa na bia hiyo, kujisajili kwa wingi ili
Milioni 20 walizotenga za zawadi zibaki Tanzania.
“Bila
shaka tunatarajia kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi ndio
maana tunasisitiza kuhusu usajili mapema ili kuepuka usumbufu dakika za
mwisho,” alisema huku akiwapongeza waandaaji kwa maandalizi mazuri huku
wakazi wa Dar es Salaam wakipewa nafasi ya kujisajilipia Februari 24 na
25 katika viwanja vya Mlimani City.
Alisema
wao kama wadhamini wakuu pia watatoa milioni moja kwa mTanzania wa
kwanza wa katika mbio za kilometa 42 na milioni moja pia kwa mwanamke.
“Hii nimojawapo ya njia za kuongeza hamasa katika mbio hizi ambazo miaka
ya nyuma zimetawalwa na Wakenya.
Naye
kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alitoa wito
kwa washiriki wote wa kilometa 21 kuanza maandalizimapema
ikiwemokujisajili tayari kwa mbio hizo zitakazofanyika Moshi Machi 4
katika Cuo Kikuu cha UshirikaMoshi (MoCU).
“Mbio
zetu za kilometa 21 zimekuwa maarufu zaidi na tunasisitiza kuhusu
kujisajili mapema ili tuwe na washiriki wengi zaidi mwaka huu na
kuendelea kutuunga mkono Tigo katika kufanyambioza kilometa 21 kuwa
maarufu zaidi,” alisema na kuongeza kuwa wametenga milioni11 kwa ajili
ya zawadi.
Meneja
Masoko wa Grand Malt, Warda Kimaro ambaye kinywaji chake kinadhamini
mbio za kilometa 5maarufu kama fun run, alisema mbiohizi zimekuwa
maarufu sana kwani zinahusisha watu wa rika zote huku akiwataka
wajisajili mapema kabla ya kufika Moshi ili waepuke usumbufu.
Wadhamini
wengine katika mbio hizi ni First National Bank, Kilimanjaro Water,
Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,
Simba Cement, KNAUF Gypsum na AAR as ambao ni wabia katika masuala ya
tibabu.
Usajili
Arusha utafanyika Februari 27 na 28 katika hoteli ya Kibo Palacekuanzia
saa nane mchana hadi saa kumi na moja na Moshi ni Machi 1 kuanzia saa
sita mchana hadi saa moja usiku, Machi 2 kuanzia saa nne asubuhi hadi
saa moja jioni na Machi 3 kuanzia saa tatu hadi saa sita mchana.
Kilimanjaro
Marathon, ambayo mwaka huu itafanyika Machi 4 katika viwanja vya MoCU,
huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa kitaifa na
kampuni ya Executive Solutions.
0 comments:
Post a Comment