Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel Maganga, alisema Wakimbizi akiwa amembeba mmoja wa watoto wa wakimbizi kutoka Burundi wakati wa kuwarejesha makwao kwa hiati ambapo wakmbizi 301 wameanza kurejea katika Mkoa wa Ruyigi na Bujumbur.
Viongozi mblimbali kutoka Serikali ya Tanzania na Burundi wakimsikiliza Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony
Laizer, ambaye aliwaeleza kuwa kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na
kati ya hao watu 12,000 wameomba kurudishwa makwao.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
UTEKELEZAJI wa makubaliano yaliyofikiwa hivi
karibuni jijini Dar es Salaam baina ya pande tatu za serikali ya Tanzania,
Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakurejesha
wakimbizi wa Burundi wapatao 12,000
umeanza utekelezaji.
Katika utekelezaji huo kwa awamu ya kwanza
Wakimbizi 301 waliokuwa wakiishi katika kambi
ya Nduta Wilayani Kibondo, walioomba kerejea Nchini mwao kwa hiyari wameanza
kurejeshwa makwao baada ya kujiridhisha kwa kuwepo hali ya amani.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya
kuwakabidhi Wakimbizi hao kwa Naibu waziri wa mambo ya ndani ya Nchini Burundi
, katika Mpaka wa Mabamba Wilayani
Kibondo, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel Maganga, alisema Wakimbizi wanaoanza
kurejea ni kutoka Mkoa wa Ruyigi familia
60 na Bujumbura familia 37 .
Alisema kikao walicho kaa wiki iliyopita cha pande tatu kiliamua Wakimbizi waliomba
kurejeshwa Nchini mwao warejeshwe na
kwasasa wao kama serikali ya Tanzania wameanza kuwarejesha na kuwakabidhi kwa
serikali ya Burundi wakimbizi 301 na
hadi mwezi wa tisa wanatarajia kuwarejesha wakimbizi 6,000 na wengine
watawarejesha mwezi wa kumi na mbili mwaka huuu.
Aidha Maganga aliwaomba Wakimbizi hao kuanza
kujitokeza kurejea mapema na wasisubiri kuondoka kwa mrundikano hali inayoweza kuwapa
ugumu katika usafirishwaji hivyo waanze kuondoka mapema.
Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony
Laizer, alisema kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na
kati ya hao watu 12,000 wameomba kurudishwa makwao na kuchelewa kurudishwa kuna
pelekea sasa hali ya usalama kuwa si nzuri kwani kunawepo na vitendo vya vurugu
za mara kwa mara kutoka kwa wakimbizi hao wanaotaka kuondoka.
"Urejeshwaji wa Wakimbizi hawa utasaidia kuwepo
na usalama na amani katika kambi maana kuna wakimbizi wengi walikuwa wakiomba
kurejeshwa kwao ninaamini hatua hii itasaidia kuwapa nguvu wakimbizi wengine
kuendelea kuamini kuwa Nchini mwao kunaamani na zoezi hili litakuwa muendelezo
kwa kambi zote", alisema Tony.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya ndani
ya Nchi ya Burundi ,Therence Ntahiraja
alisema wao kama Viongozi wa Burundi wamejipanga ipasavyo katika kuwapokea
Wakimbizi na Watawakabidhi mali zao kama walivyokuwa mwanzoni na Watawapatia
Maeneo ya kufanyia shughuli zao ilikuweza kuendesha maisha yao kama ilivyo kuwa
mwanzo.
Alisema kwasasa Nchi ya Burundi ina amani na
kuwaomba wakimbizi wote warejee Nchini mwao iliwaweze kufanya shughuli za
maendeleo na kuhakikisha Nchi yao inakuwa kiuchumi.
Nao baadhi ya Wakimbizi waliokuwa wakirejea
Nchini mwao, akiwemo Isabera
Niyonkuru walisema Wanafuraha sana
kurejea Nchini mwao na hatua hiyo itawawezesha kufanya shughuli mbali mbali na
kuweza kuzitunza familia zao na kuepukana na kuwa wakimbizi.
" tunafurahi sana kuona serikali ya
Tanzania imetutunza kwa kipindi chote tulichoishi Nchini humo tunawashukuru
sana, tunaamini tunaporejea nyumbani kwetu tutapokelewa na kuishi kwa amani na
tunaomba wasichoke kutusaidia tutakapokuwa na matatizo", alisema
Niyonkuru.
0 comments:
Post a Comment