Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo (wa
pili kulia) akiongea kwa simu na moja ya washindi wa promosheni ya
Jishindie na DStv iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania
jijini Dar es Salaam leo.
Wengine ni Abdalla Hemed Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya
kubahatisha Tanzania, Ronald Shelukindo (wa pili kushoto) Meneja
Operesheni wa Multichoice na Erick Mosha ni wa kitengo cha Uhifadhi
wateja Multichoice Tanzania. Takriban washindi 200 wamejishindia
zawadi mbalimbali kwenye promosheni hiyo ikiwemo safari ya kutalii
Zanzibar kwa familia mbili.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo
(katikati) akifurahia jambo na Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya
kubahatisha Abdallah Hemed (Kushoto) na afisa wa uhifadhi wateja wa
Multichoice Tanzania Erick Mosha
wakati wa droo ya promosheni ya Jishindie na DStv iliyofanyika leo
katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam. Takriban
washindi 200 wamejishindia zawadi mbalimbali kwenye promosheni hiyo
ikiwemo safari ya kutalii Zanzibar kwa familia mbili.
******************
Wateja
76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania
katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa
DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake
kwa angalau miezi miwili mfululizo.
Kati ya
washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora
ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi
wawili wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 169,000)
cha mwezi, wengine wawili Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 109 000), huku
washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 69,000), 10
kifurushi cha Famili (39,000) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh
19,000.
Washindi
wawili wa droo kubwa ambao ni Anicet Macheta waKagera na Hassan Juma
Hassan wa Dar es Salaam wamejishindia zawadi kubwa kabisa ambayo ni
safari ya kutalii visiwani Zanzibar wao pamoja na
familia zao zisizozidi watu wane kila familia.
Akizungumza
baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ya mwisho leo hii katika ofisi za
Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo
amebainisha kuwa zaidi ya wateja 30,000 wameshiriki
kwenye promosheni hiyo iliyoendelea kwa miezi miwili.
Hilda
amesema, wamefurahi kuona kuwa washindi takriban 200 waliopatikana
wakati wote wa promosheni wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo
Arusha, Mwanza Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro,
Kigoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na mikoa mingine kote nchini.
“Wakati
wote DStv tunahakikisha kuwa wateja wetu wanafurahia huduma zetu kwani
mbali na kwamba sisi ni vinara katika burudani na michezo, pia tunakuwa
na promosheni za mara kwa mara ambapo wateja
wetu hupata zawadi mbalimbali” alisema Hilda.
Amesema
kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa wateja wa DStv kwani mbali na
kuongeza chaneli kwenye vifurushi hususani vile vya bei ya chini, pia
hivi majuzi DStv ilipunguza bei za vifurushi vyake
vyote ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata huduma hizo
kwa unafuu mkubwa.
Kampuni ya
Multichoice Tanzania inayoendesha biashara ya vingamuzi vya DStv, ina
umri wa miaka 20 sasa ambapo ilianza shughuli zake hapa nchini mnamo
mwaka 1997.
0 comments:
Post a Comment