Katibu wa Afya, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Stella Mwakikunga, ambaye pia ni Mkufunzi katika Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nakuwahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.Picha:Mroki Mroki-DAILY NEWS Digital.
TANZANIA imetajwa kuwa nchi iliyofanikiwa kuwa
na mfumo wa Kielektroniki uliojengwa na wataalamu wake wa ndani wenye uwezo wa
kuunganisha vituo vya kutolea huduma kama Zahanati ,Shule, Vituo vya Afya na Hospitali
zote nchini hali itakayowezesha kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa kwa
wananchi katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Mtaalam wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Desderi Wengaa
kuwa Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa na wataalamu wenye uwezo wa
kujenga mifumo ya kielektroniki itakayosaidia kuchochea maendeleo.
“Tanzania imekuwa nchi ya mfano Afrika Mashariki,
Kusini mwa Afrika na Afrika kwa kuwa na
mfumo unaowezesha wananchi kutoa mrejesho wa
huduma wanazopata katika maeneo ya kutolea huduma hali itakayoongeza
uwazi na uwajibikaji,” alisema Wengaa.
Mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa PlanRep
yanawahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu,
na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora.
Mikoa minginine nchi nzima tayari imeshapatiwa
mafunzo hayo ambapo uzinduzi rasmi wa matumizi yake unataraji kufanyika mapema
mwezi huu.
Mradi wa PS3 unatekelezwa na Ofisi ya Rais –
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na umejikita katika maeneo ya Utawala
Bora na Ushirikishwaji wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha, Mifumo ya
TEHAMA pamoja na Tafiti Tendaji, Tathimini na ufuatiliaji.
Washiriki wa Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanawahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, wakiendelea na mafunzo hayoleo katika siku ya nne mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Ofisa kutoka Tamisemi, Ayoub Kambi ambaye pia ni Mkufunzi katika Mafunzo
ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za
Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) na kuwahusisha Waganga Wakuu wa
Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa
Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa
mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.
Mkufunzi Christopher Masaka akifundisha namna ya uendeshaji wa Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za
Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) na kuwahusisha Waganga
Wakuu wa
Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa
Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa
mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.
Washiriki
wa Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na
Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanawahusisha Waganga
Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na
Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na
Tabora, wakiendelea na mafunzo hayoleo katika siku ya nne mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment