Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2017

Afisa muandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah (katikati waliokaa)akifuatilia kwa karibu wakati wa droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv ambapo wateja takriban 100 wa DStv walijishindia zawadi mbalimbali. Kulia ni Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, Wengine ni maafisa wa Multichoice Erick Mosha (aliyesimama) na Leyla Partick.
 Afisa muandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah (kulia) akifuatilia kwa karibu wakati wa droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv ambapo wateja takriban 100 wa DStv walijishindia zawadi mbalimbali. Katikati ni Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo na kulia ni Meneja wa Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Barka Shelukindo.WATEJA 76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika promosheni inayoendelea ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa mangalau miezi miwili mfululizo.

 Kati ya washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi watatu wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 184,000) cha mwezi mmoja, wengine watatu Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 122 500), huku washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 82,250), 10 kifurushi cha Famili (42,900) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,975.

Promosheni hii inaendelea kwa muda wa miezi miwili itatoa washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo vifurushi vya muda wa matangazo, ving’amuzi, pamoja na zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar kwa washindi wawili pamoja na familia zao.

 Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza leo hii katika ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa Zaidi ya wateja elfu 10 wameshiriki kwenye droo hiyo  hii ikionyesha muitikio mkubwa wa wateja.

Pia amebainisha kuwa washindi waliopatikan katika droo ya kwanza wametoka kila pembe ya nchi ikiwemo Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

Amewataka wateja wa DStv kuendelea kulipia ving’amuzi vyao kwani bado droo moja kubwa ya mwisho ambapo kuna wateja wawili watakaoshinda safari ya kutalii Zanzibar pamoja na familia zao.

Amesema promosheni hiyo haina ugumu wa kushiriki kwani anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia kifurushi chochote kile cha DStv na kisha kuendelea kutumia huduma hiyo na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo zitakazochezeshwa kila baada ya wiki mbili. Droo kubwa ya mwisho tarehe 1/9/2017.
Posted by MROKI On Wednesday, August 02, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo