Nafasi Ya Matangazo

July 24, 2017

WAJUMBE wa Umoja wa Afrika wa  mapambano dhidi  ya rushwa katika  nchi wanachama wa Afrika wameapisha wajumbe wapya wa bodi ya hiyo ambao watahamasisha mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi hizo.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa Mjumbe wa bodi hiyo kutoka Tanzania ambaye pia ni mwakilishi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania, Sabina Seja alisema kuwa, bodi hiyo itasaidia kupambana na rushwa kwenye nyanja mbalimbali.

Alisema kuwa, kazi kubwa ya bodi hiyo ni kuweza kupitia mikataba mbalimbali kwenye nchi wanachama lakini pia kuhakikisha kuwa wanapiga vita vitendo vya rushwa kwenye mikataba hiyo kwani rushwa ni adui mkubwa kwenye nchi hizo.

Alisema kuwa,bodi hiyo ina wanachama kumi na moja ambapo mpaka sasa hivi ni wanachama kumi tu waliopo kutoka nchi tofauti na watahamasisha nchi hizo  wafuate sheria zilizopo na kuwepo kwa ufuatiliaji wa Karibu na kupunguza maswala ya rushwa.

Aidha akielezea hali halisi ya mapambano ya rushwa katika nchi hizo, alisema kuwa, tatizo la rushwa kwa nchi hizo bado ni kubwa lakini viwango vya rushwa vinatofautiana baina ya nchi na nchi nyingine  huku vitendo hivyo vikiathiri uchumi wa nchi hizo kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wa Mjumbe wa bodi aliyeapishwa kutoka nchini, Namibia Noa  Paulus alisema kuwa, kuapishwa kwa bodi hiyo kutasaidia sana kupunguza tatizo la rushwa kwa nchi hizo na kuchochea uchumi wa nchi husika.

"bodi hii ya wajumbe walioapishwa Leo naamini kuwa itafanya kazi kubwa katika kuhakikisha mikataba iliyopitishwa dhidi ya mapambano ya rushwa ili tuweze kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa kubwa katika nchi za Afrika na linachangia kuzorotesha maendeleo na uchumi."alisema Noa.
Posted by MROKI On Monday, July 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo