Mkurugenzi
wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Women Tears Ltd, Doreen Kimbi
akikabidhi misaada ya mablankenti kwa wazee mbalimbali wa Moshi Vijijini
hivi karibuni ikiwa ni saada wa asasi hiyo kwa wazee hao wa;lio na
mahitaji mbalimbali. Zaidi ya wazee 200 walinufaika na misaada hiyo.
Mkurugenzi
wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Women Tears Ltd, Doreen Kimbi
akikabidhi misaada ya mablankenti kwa wazee mbalimbali wa Moshi Vijijini
hivi karibuni ikiwa ni saada wa asasi hiyo kwa wazee hao wa;lio na
mahitaji mbalimbali. Zaidi ya wazee 200 walinufaika na misaada hiyo.
ZAIDI ya wazee 214 wa Moshi
Vijijini ambao wanaotegemea msaada wa
matibabu na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu kutoka kwa wasamaria wema kwa
ajili ya kujikimu kimaisha, wamepatiwa msaada wa jora tatu za nguo za baridi,
baada ya kufadhiliwa na asasi isiyo la kiserekali la Women Tears Limited.
Mkurugenzi wa Shirika hilo,
Doreen Kimbi alisema pamoja na mambo mengine kundi jingine la wazee
watakaotambuliwa na asasi yake wataanza kunufaika na uchunguzi wa afya
utakaofanywa na jopo la madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
“Kuna mabadiliko makubwa ya
hali ya hewa kwenye mkoa wetu, hasa ongezeko la baridi katika Wilaya ya Moshi
na miji ya jirani, wanaopata tabu, wengi wao ni wazee hawa ambao wanategemea
misaada ya kibinadamu. Kama Shirika ambalo linashughulika na kundi hili,
tumeamua kutoa majora matatu yenye masweta kwa wazee zaidi ya 214 ili
wajisitiri,”alisema Doreen
Alisema licha ya shirika hilo
kutokuwa na wafadhili kwa sasa lakini amelazimika kutoa fedha zake mfukoni ili
kuwasaidia wazee hao kutoka vijiji vya Kitandu Mkwaleni, Kitandu Minja na
Kitandu Shinga vilivyopo Kata ya Uru Kusini.
Kuhusu uchunguzi wa afya,
Mkurugenzi huyo alisema bado anahaha kutafuta fedha kwa wafadhili mbalimbali
kwa ajili ya kuendesha zoezi maalumu la uchuguzi huo bila malipo, kwa kuwa
idadi kubwa ya wazee wasiojiweza wanasumbuliwa na saratani ya tezi dume,
kisukari na magonjwa ya moyo.
Shirika hilo limesisitiza pia
kwamba liko tayari kuwawezesha wazee hao kufikia gharama za matibabu kwa
kuwakatia vitambulisho vya Bima ya Afya ya Jamii (CHF).
Mbali ya kusaidia wazee, pia
shirika hilo linapigana kutoa elimu kwa raia kuachana na ukatili na mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albinism).
Wakati wazee wasiojiweza
wakihitaji misaada kadha wa kadha, bado taifa lina deni kubwa la changamoto ya
kukwama kwa miaka 14, sera ya taifa ya wazee ya mwaka 1999 ambayo haijapelekwa
Bungeni kutungwa na kuwa Sheria.
Mkwamo ambao unatajwa kama
udhaifu unaochangia kushamiri kwa matukio ya ukatili na kutojumuishwa kwa wazee
hao katika ajenda ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment