Kamati ya Olympic Duniani
imeipa tena SuperSport kibali cha kurusha matangazo ya michuano ya Olympic
kuanzia mwaka 2018 hadi 2024 barani Africa Kusini mwa jangwa la Sahara.
Makubaliano hayo kati ya
kamati hiyo (International Olympic Committee IOC) yanamaanisha kuwa Supersport
imepata haki ya kurusha michuano hiyo katika eneo hili la Africa. Michuano hiyo
ni pamoja na ile ya PyeongChang 2018,
Tokyo 2020, Beijing 2022 na ile ya mwaka 2024 ambayo bado haijaamuliwa
itafanyika katika nchi gani.
Tangazo hilo limetolewa baada
ya kukamilika kwa mchakato wa kutoa zabuni kwa warusha matangazo katika kanda
hii ya Afrika - Kusini mwa Sahara. Kwa
minajili hii, SuperSport pia itashirikiana na IOC katika kusaidia na kuongeza
ufahamu na umaarufu wa michuano hiyo barani Africa.
Rais wa IOC Thomas Bach
amekarikiwa akisema: “Tunafurahi sana kufanya kazi tena na DStv SuperSport
hususan katika kuwahakikishia wapenzi wa michuano hii fursa ya kuishuhudia
popote walipo katika kanda hii ya Afrika – Kusini mwa Sahara.
Binafsi
nimetembelea nchi mbalimbali barani Afrika na nimeshuhudia ushabiki mkubwa
uliopo kwa michuano hii. IOC hutumia asilimia 90 ya mapato yake ya tokanayo na
mikataba ya kibiashara katika kuendeleza michezo kote duniani ikiwemo Afrika”.
Naye Gideon Khobane, Afisa
Mkuu wa SuperSport amesema “Sisi tukiwa
kama wadau wa muda mrefu na washirika wa
IOC, tumefurahi sana kuingia makubaliano haya na mdau wetu. Michuano hii
inawatazamaji wengi sana kutokana na
umaarufu wake na umahiri mkubwa wa kimichezo unaoonyeshwa na hivyo kuwa kivutio
kikubwa sana kwa watazamaji.
Tunaimani kwa kupitia DStv SuperSport, tunawapa
haki mamilioni wa washabiki wa michezo barani Afrika fursa ya kushuhudia michezo
ya Olympic, moja ya mashindano makubwa kabisa duniani na yenye msisimko
mkubwa”.
SuperSport ni manguli wa
kurusha matangazo ya michezo barani Afrika. SuperSport ina chaneli 37
zinazorusha matangazo ya michezo mbalimbali kuanzia michezo mikubwa kama vile kandanda pamoja na
michezo midogomidogo na ile inayochipukia. Supersport huonekana katika nchi 54
Afrika – kusini mwa sahara pamoja na visiwa vya jirani.
0 comments:
Post a Comment