SHIRIKA la ndege la Kitanzania
Precision Air leo imezindua kwa mafanikio safari zake za kwenda Entebbe.
Ndege ya uzinduzi wa
safari hizo iliondoka Jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:10 asubuhi kuelekea
Entebbe na kuwasili Entebbe majira ya saa 4:50 Asubuhi na kupokewa kwa salamu
maalumu ya kumwagiwa maji na magari ya zima moto, ikiwa ni ishara ya kuanza
rasmi kwa zama mpya za huduma za Precision Air kati ya Tanzania na Uganda.
Akizungumzia kuanza
rasmi kwa safari hizo Meneja Uratibu na Mahusiano Bw. Hillary Mremi amesema
kuwa, kupitia safari za Precision Air Tanzania na Uganda wamehakikishiwa
usafiri wa uhakika.
“Tutakuwa tukifanya
safari mara tatu kwa wiki, kila siku ya Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi na
baadaye kuongeza safari kulingana mahitaji ya soko.” Amekaririwa Bw. Mremi
Precision Air iliahirisha
safari za Entebbe mnamo mwaka 2013 kupisha maboresho ya mtandao wa wa safari
zake katika kuhakikisha inazingatia tija
katika shughuli zake.
Precision Air ndilo
Shirika pekee la ndege linalotambuliwa na IATA ambalo linafanya safari za moja
kwa moja kati ya Tanzania na Uganda. Inatarajiwa safari hizi za Precision zitaimarisha
mahusuano ya kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda, hasa
ikizingatiwa kuwepo kwa miradi mbali mbali ya pamoja kama ule wa bomba la
mafuta litakalo anzia nchini Uganda hadi Tanzania.
Ni miradi kama hiyo
inayotarijiwa kunufaika na safari za Precision Air kwa kufanikisha miradi hiyo kwa wakati.
Precision
Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za
kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya
mashirika ya ndege ya nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa
sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11.
Iktokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha,
Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar na
Nairobi.
0 comments:
Post a Comment