Wasanii wanaoshiriki katika Tamithilia ya HUBA wakiwa katika mapozi mbaluimbali.
ILE tamthilia
kabambe ya Huba inayoonyeshwa kupitia DStv katika chanel ya Maisha Magic Bongo
inaendela tena baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa tamthilia hiyo mwezi
Machi mwaka huu.
Huu ukiwa ni msimu
pili, tamthilia hiyo ambayo imeainishwa kama moja ya tamthilia maarufu zaidi
ukanda wa Afrika Mashariki, imeanza kwa kishindo kutokana na kuongezwa kwa
vionjo na pia washiriki maarufu wa filamu hapa nchini.
Tamthilia ya Huba
huigizwa hapa nchini na waigizaji wa hapa hapa nchini akiwemo Rammy Gallis
(Dev), Riyama Ali, Muhogo Mchungu, Grace Mapunda (Tesa) na Aunt Ezekiel (jojo)
ambaye ni muigizaji mpya katika tamthilia hii.
Akizungumzia ujio wa
msimu wa pili wa Huba, Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo Barbara Kambogi
amesema tangu kuanza kwa tamthilia hiyo ya Huba.
Mwezi Novemba mwaka
jana imefanikiwa kuliteka soko la tamthilia hapa Afrika Mashariki na kuifanya
kuwa moja ya tamthilia matata kabisa katika soko la Afrika Mashariki.
“Kwa mara ya kwanza
katika historia ya filamu na hususan tamthilila Watanzania tumefanikiwa kuiweka
tasnia yetu ya uigizaji filamu katika ramani ya kanda ya Afrika Mashariki na
bara zima kwa ujumla kutokana na ufanisi wa tamthilia yetu ya Huba ambayo
inatayarishwa hapa nchini na kuigizwa na watanzania wenyewe” alisema Barbara.
Amesema kuwa kwa
ufanisi uloonyeshwa na tamthilia hiyo katika msimu wa kwanza, wanatarajia kuwa
msimu huu wa pili utakuwa wa kuvutia zaidi hasa ikizingatiwa kuwa waigizaji
wote wameiva visuri zaidi, vionjo vimeongezwa na pia waigizaji wengine wapya
akiwemo Anti Ezekiel ambaye ni miongoni mwa waigizaji maarufu hapa nchini “Sisi
DStv, na hususan channel yetu ya Maisha Magic Bongo, tulisikia kilio cha muda
mrefu cha Watanzania wengi waliokuwa wakitutaka kuongeza maudhui ya Kitanzania,
na hatimaye tukaamua kuanzisha chaneli maalum yenye maudhui kutoka Tanzania. Na
sasa tunaendelea kuiboresha chaneli hii ya Maisha Magic Bongo na maudhui yake
kwa ujumla hivyo watanzania wasiache kutazama chanel hii kwani ni yetu” alisema
Barbara.
Tamthilia ya Huba
katika chanel ya Maisha Magic Bongo inapatikana katika vifurushi vyote vya DStv
kikiwemo kile cha DStv Bomba kwa shilingi 19,975 tu kwa mwezi kikiwa ni moja ya
vifurushi vya bei nafuu kabisa sokoni.
Msimu huu wa pili
wa huba unatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa na tamthilia hiyo huoneshwa
katika chanel ya Maisha Magic Bongo (DStv 160) kila siku za Jumanne na Jumatano
saa moja na nusu usiku.
0 comments:
Post a Comment