Watuhumiwa James Rugemalila
(kulia) na Harbinder Sethiwakiwa
chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi na Magereza kabla ya kupandishwa
kizimbani katika Mahakam ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Watuhumiwa James Rugemalila
(kushoto) na Harbinder Sethi wakiwa
chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi walipofikishwa kizimbani katika Mahakam ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
******************
WAFANYABIASHARA maarufu nchini, James Rugemalila
na Harbinder Sethi wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo
kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni 22.1 na Sh
bilioni 309. Anaandika Fransisca Emmanuel
wa Habarileo.
Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kusomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Paul Kadushi anayesaidiana na Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja
Nchimbi na Joseph Kiula wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).
Mashitaka yao ni kula njama, kujihusisha na
mtandao na uhalifu, (kughushi na kutoa fomu zilizoghushiwa (yanamkabili Seth)
kujipatia fedha kwa udanganyifu na kusababisha serikali hasara.
Rugemalila
na Seth wamekosa dhamana hivyo wanaenda mahabusu hadi kesi yao
itakapotajwa tena kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, haina
mamlaka ya kusikiliza mashitaka ya uhujumu uchumi hivyo maombi ya
dhamana yanatakiwa kupelekwa Mahakama Kuu.
0 comments:
Post a Comment