Mkaguzi wa Polisi wa wilaya ya Korogwe,
Merkiad Makumba akikata utepe wakati wa kuzindua duka la Airtel katika
wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, akishuhudia ni Afisa wa wateja wa Airtel
Korogwe, Bi Elen na
Meneja mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango.
*************
Wakati
uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani,Jamii imetakiwa
kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia jeshi la polisi kubainisha
watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya kutekeleza
haki yao ya kikatiba
Wito
huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi Merkiad Makumba jana kwa niaba ya
Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa
la kampuni ya simu za mkononi la
Airtel katika wilaya hiyo mkoani Tanga
Hatua
hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo ambavyo
vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi Makumba.
“
Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa
wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa
sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi
Mkumba
Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.
Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.
Kiango
aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili
line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na
huduma za intaneti na nyingine
nyingi , aidha alitumia fursa hilo kuwakaribisha wakazi wa Korogwe
kulitembelea duka hilo.
Mpaka
sasa Airtel imeshazindua maduka mengine kama hili katika mikoa ya
Shinyanga, Dodoma, Arusha , Manyara , Dar na Morogoro.
Mpango huo wa
kuzindua maduka ya kutoa hudma kwa wateja
unalenga kupanua na kusogeza huduma za AIRTEL karibu na jamii hivyo
kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi muhimu na kutatua changamoto za
wateja kwa urahisi na haraka zaidi. Mpaka ifikapo mwisho wa mwaka
Airtel itazindua zaidi ya maduka 2000 nchini
0 comments:
Post a Comment