Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , Nuru Millao
(kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini , Roeland Van De Geer (kulia)
wakifunua kitambaa kuonyesha jiwe la msingi linaashiriwa kufunguliwa kwa Kituo
cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo katika jengo la Old
Boma leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo, Nuru Millao akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo
Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla ya kufungua kituo cha Urithi wa
Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo
katika jengo la Old Boma leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya
Mwita akiongea na wageni (hawapo katika picha) wakati wa hafla ya kufungua Kituo
cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo katika jengo la Old Boma leo Jijini Dare s Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao
(mwenye mtandio) akiwa katika picha na wageni waliohudhuria hafla ya ya
kufungua kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo kilichopo katika jengo la Old Boma
na Utalii leo Jijini Dar es Salaam.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo , Nuru Millao
ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa
kulifanya jengo la Old Boma kuwa Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na
Utalii (DARCHI).Anaandika Lorietha Laurence- WHUSM.
Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo
hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, Millao alisema hatua hiyo
inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania
unadumishwa na kukuzwa.
“Ni dhahiri kuwa wananchi wataweza kufahamu umuhimu wa kutunza na
kuhifadhi majengo ya kale kutokana na elimu watakayoipata kupitia kituo hiki
katika kukuza utamaduni ” alisema Millao.
Aidha alitoa wito kwa kwa Jumuiya ya Wasanifu
Majengo Tanzania kuendelea kushirikiana na Taasisi za ndani na nje ya nchi
katika kutekeleza mipango ya kutunza majengo na sehemu za kale ili kuhifadhi historia na utamaduni wa Mtanzania.
Pia amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa
katika Jiji la Dar es Salaam kusimamia sheria kwa kushughulia kero mbalimbali zinazotokana na
udhaifu wa sheria za kuendeleza majengo ya kale.
Naye
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameeleza kuwa
kufunguliwa kwa kituo hiko ni fursa ya
kukuza pato la uchumi wa nchi kupitia mapato ya watalii watakaokitembelea.
“Tayari
tumeweka mipango mbalimbali ya kuhakikisha Jiji letu la Dar es Salaam linakuwa
sehemu ya Utalii kwa kutoa mafunzo kwa madereva Taxii ambao wanahusika katika
kuwasafirisha watalii ili wawe na uelewa
zaidi kuhusu kituo hiki ” alisema Mstahiki Meya Mwita.
Kwa Upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini,
Roeland Van De Geer amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana kwa karibu na
Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla katika kuleta maendeleo.
0 comments:
Post a Comment