Msajili
wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano (kushoto)akikata utepe ikiwa ni
ishara ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Benki ya TPB,kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu TPB,Sabasaba Moshingi ,ambapo ofisi hiyo mpya ipo
katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akizindua jiwe la msingi katika benki ya TPB iliyopo eneo la Mwanjelwa.
Msajili
wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindanoakizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa jengo jipya la ofisi ya benki ya TPB Mwanjelwa.
Afisa
Mtendaji Mkuu TPB SabaSaba Moshingi ,kushoto akimkabidhi ripoti ya
Mwaka Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano katika hafla ya uzinduzi
wa ofisi mpya ya jengo la Tpb Mwanjelwa jijini Mbeya.
Msajili
wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akionesha kadi maalum
aliyokabidhiwa na benki ya TPB mara baada ya kuzindua jengo hilo la
ofisi eneo la mwanjelwa jijini Mbeya.
Meza kuu katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa TPB.
***********
TAASISI
za kifedha nchini, zimetakiwa kuboresha mifumo ya utendaji kazi, ili kwenda
sambamba na mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.
Kauli
hiyo, imetolewa leo na Msajili wa Hazina
Dkt .Osward Mashindano, wakati akizindua Ofisi kuu ya Benki ya TPB iliyoko katika eneo la Mwanjelwa Jijini
Mbeya.
Amesema,
wakati uchumi wa dunia unakua ni vema taasisi hizo zikajiimarisha kiutendaji
ili kukidhi vigezo vya ushindani wa
kibiashara ndani na nje ya nchi.
“Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta za
kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo ni
wakati wenu nanyi kubadili mifumo ya utendaji kazi ili kwenda sambamba na
ukuaji huo wa uchumi“,alisema.
Aidha
ametoa wito kwa taasisi za kifedha nchini kuhakikisha inaweka mazingira rafiki
kwa wananchi wa kipato cha chini kwa kuweka gharama nafuu za huduma zao ili
waweze kuzimudu.
Pia, Mashindano ameipongeza benki ya TPB kutokana na na jitihada zake za
kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na
mawakala.
Hata
hivyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo imetoa
gawio kwa serikali kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 ambapo hundi hiyo inatarajiwa
kukabidhiwa mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment