Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki, akitoa hotuba ya ufunguzi wa
mkutano wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini
mwa Afrika, (SARPCCO) ikiwa ni
maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa
kufanyika Mei 24,2017 mkoani Arusha.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.
Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa
nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika jumatano Mei 24, 2017
mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Taarifa
iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa
Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na
Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa
na
Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho
la
Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho
hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo
mkuu.
Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa
ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni
za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji
haramu wa binadamu na ugaidi.
“Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio
yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za
sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao
uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.
SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa
Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo
vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania,
Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika
Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.
0 comments:
Post a Comment