Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mongella amewasisitizia
wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili
kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Umoja wa
Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, akizungumza hii leo kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika
kitaifa Jijini Mwanza.
Afisa Habari na Utafiti
kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania,
Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini
Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia), akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016". Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Uzinduzi wa "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya
hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.
Akizungumza
mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru
wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku
akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya
habari za kihisia.
Afisa
Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)
tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo
imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31,
2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC.#BMGHabari
0 comments:
Post a Comment