Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.

Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, ambaye amemwakilisha Rais John Pombe Magufuli

Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia), akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016". Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Uzinduzi wa "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.
 
Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia. 

Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC.#BMGHabari

Posted by MROKI On Wednesday, May 03, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo