Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (mwenye bahasha mkononi) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF pamoja na wanachama waliopo nchini baada ya kuhitimisha zoezi hilo siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam
*************************
Wanachama
wa chama cha Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) wamejipatia
uongozi mpya baada ya kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi siku ya Jumapili
Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar
es salaam. Jumla ya wanachama hai na halali 41 walishirki katika
uchaguzi huo, ambapo wanachama 23 walikuwepo ukumbini na wanachama 18
waishio nje ya nchi walipiga kura kwa njia ya mtandao.
Bw.
Alkarim Bhanji alishinda nafasi ya Uenyekiti akiwa mgombea pekee,
wakati Bw. Mohamed Irapo alinyakua nafasi ya Makamu Mwenyekiti. Katibu
Mkuu wa kipindi cha mpito Bw. Wahid
Abdulghafoor aliweza kutetea kiti chake akiwa mgombea pekee. Nafasi ya
Katibu Mkuu msaidizi imechukuliwa na Bw. Fabian Kimongw wakati Bw.
Bakari Simba ametetea tena nafasi ya Mweka Hazina Msaidizi aliyokuwa
akishika wakati wa kipindi cha mpito.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa umesimamiwa vyema na Katibu Mkuu wa klabu ya
michezo ya Saigon, Bw. Boi Juma, jumla ya wajumbe watano kati ya sita
wanaotakiwa kikatiba walichaguliwa. Hao ni Bw. Shaaban Kessy Mtambo, Bw. Abdallah Kizua, Bw. Idrissa Jumbe, Bi. Sophia Muccadam na Bi. Salma King.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa KFDF Bw. Wahid
Abdulghafoor, nafasi mbili za Mweka Hazina na Mjumbe mmoja zilizo wazi
baada ya kutotokea mgombea zitajazwa baadaye katika uchaguzi mdogo.
KFDF ni chama kinachojumuisha wananchi wanaoishi ama waliopata kuishi eneo lote Kariakoo, dhumuni kuu likiwa ni kuwaunganisha upya na kufanya shughuli za kijamii kimaendeleo kwa lengo la kudumisha na kuendeleza umoja, mshikamano na undugu uliokuwepo miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo maarufu la jiji la Dar es salaam toka enzi za mababu. |
Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (kati) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment