Meneja
wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka
***********
Na Mwandishi wetu
WAMILIKI na watumiaji wa
maji ya visima hususani wakazi wa Ilala jijini Dar es salaam wametakiwa
kujitokeza ili kuunganishiwa huduma ya Majisafi yanayotolewa na shirika la
Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO).
Wito huo wa Dawasco
umelenga kuwasaidia wananchi wa maeneo mbalimbali kuondokana na hujuma
inayofanywa na wamiliki wachache wa visima binafsi vya Maji dhidi yao na
shirika.
Hayo yalisemwa na Meneja
wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari juu ya mpango wa kuunganishia wamiliki wa visima katika mfumo rasmi wa
Dawasco.
Akielezea juu ya mpango
huo, Kaoneka alisema kwa kipindi kirefu kiasi cha maji kilichokuwa kinazalishwa
hakikuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wote hususani wakazi wa Ilala, hivyo
kupelekea watu wengi kuchimba visima vya maji binafsi.
“Tulikuwa na changamoto
ya utoshelezaji wa Maji kwa maeneo mengi ya mji. Uzalishaji Maji haukuwa mkubwa
hivyo kwa wananchi wengi iliwalazimu kuchimba visima vyao binafsi ili wapate
huduma hiyo,”alisema Kaoneka.
Aliyataja maeneo ambayo
yanaongoza kuwa na visima vingi kuwa ni vinavyotoa huduma ya maji safi ni na vinamilikiwa na watu binafsi kuwa ni Kariakoo,
Upanga na katikati ya Mji.
“Kwa sasa uzalishaji wa maji
umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka kiasi cha lita za ujazo milioni 182 hadi
lita za ujazo milioni 270 kwa siku, hivyo kupelekea maeneo mengi ya jiji la Dar
es Salaam kuwa na utoshelezi mwingi wa maji.
“Nitoe rai kwa wamiliki
wote wa visima katikati ya mji kuja ofisi za Dawasco ili kujiunga rasmi na
mtandao wa majisafi. Aidha tumegugundua wengi wa wamiliki wa visima hufanya
maunganisho ya maji bila kufuata taratibu husika na mwisho hudai yale maji ni
ya kisima wakati Dawasco tukishayapima tunagundua ni ya Dawasco,” aliongeza
Kaoneka.
Aliwataka wananchi kutoa
kutoa taarifa za watu wanaohujumu miundombinu ya dawasco kwa kutoa taarifa
ktika ofisi zao mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment