Nafasi Ya Matangazo

March 22, 2017



Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro,  Dr. John Ndunguru  akifungua Mafunzo ya Maofisa Habari na Maofisa Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Tanga mkoani Morogoro juzi kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) yanahusu uanzishaji na uendeshaji wa Tovuti za Serikali.
Noel Kazimoto - AAS Lga Morogoro akizungumza.
Meneja Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) mkoa wa Morogoro, David Ole Laput akitoa maelezo ya mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara. Ila katika uboreshaji wa mawasiliano kwa umma mradi huo unashirikisha Halmashauri na mikoa yote ya Tanzania bara kwa kuwapa mafunzo maafisa habari na maafisa Tehama wa maeneo husika.

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kumalizika Machi 27 mwaka huu kwa kuzinduliwa tovuti hizo za Halmashauri na Mikoa ambapo uzinduzi wa kitaifa ni mkoani Dodoma.
Mwakilishi wa TAMISEMI - Kundasai Archbold akizungumza kuhusuana na mradi huo na manufaa yake kwa jamii na serikali.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kumalizika Machi 27 mwaka huu kwa kuzinduliwa tovuti hizo za Halmashauri na Mikoa ambapo uzinduzi wa kitaifa ni mkoani Dodoma.
Picha ya pamoja ya washiriki na mgeni rasmi ilipigwa.
Posted by MROKI On Wednesday, March 22, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo