Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akipokewa kwa furaha na mmoja wa watoto wake alipowasili nyumbani kwake hii leo akitoka mahabusu.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alipowasili nyumbani kwake hii leo.
Bety Alex, Arusha
Mahakama kuu kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa
jimbo la Arusha mjini Godbles Lema.
Lema ameachiwa kwa dhamana ya sh milioni moja
pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika na
serikali.
Akisoma hukumu ya Mbunge Lema katika Mahakama Kuu Arusha Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi amesema kuwa Mbunge Lema hakupaswa kukaa mahabusu mda mrefu kwani ilipaswa kupewa dhamana.
Jaji magimbi amesema kuwa wanamwachia lema kwa dhamana hiyo
ya milioni moja ambapo kiasi hicho kimetolewa kwa njia ya bondi huku
wadhamini wawili nao wakiwa na vigezo vya dhamana.
Akizungumza nje ya Mahakama hiyo Mbunge Lema amesema kuwa Jamhuri ilikuwa na nia ya kumfunga lakini mungu amempigania mpaka kutoka
huku akimshukuru mke wake kwa jinsi alivyomfariji kwa kipindi akiwa
ndani.
Alisema kuwa kwa sasa ameandaa waraka wa kumwandikia raisi
kuwa wapo watu wanaoteseka bila kuwa na hatia magereza na kwamba atautoa
hivi karibuni
Nae wakili mtetezi wa Lema, Peter Kibatala alisema
kuwa Mahakama kuu imelekeza kuwa mahakama za chini zisimamie madaraka
yake na mamlaka yake bila kuyaachia na hivyo kwa sasa wanatakiwa
kujiandaa kwa ajili ya kupambana na kesi.
Nae Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe alisema kuwa
wanamkaribisha tena Lema Bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza
vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali
waliofika kutetea dhamana ya lema.
Aidha Mbowe amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi
kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwapiga wananchi bila makosa kwa madai
kuwa wanakuja kuleta vurugu huku lengo ni kuja kusikiliza mbunge wao.
0 comments:
Post a Comment