Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti amewataka Wakuu wa Shule Wilayani humo pamoja na Wazazi kuhakikisha wanatunza madawati waliyo kabidhiwa pamoja na kukomesha utoro wa Wananfunzi. Aidha, aliwataka Kuhakikisha ufaulu wa Wanafunzi unaongezeka kutoka asilimia 74.3 kufikia asilimia 84% kutokana na Miundombinu ya kufundishia kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kutatua suala la upungufu wa madawati.
Rai hiyo aliitoa jana wakati akikabidhi madawati 1600 kwa wakuu wa Shule 50 zilizokuwa na upungufu wa madawati katika Shule ya Msingi Buhigwe ambapo aliwaomba kuhakikisha wanayalinda madawati hayo yasiharibiwe pamoja na kuhakikishi wanafunzi wote wanahudhuria Shuleni kwasababu changamoto kubwa iliyokuwa ikichangia elimu kushuka ni pamoja na wanafunzi kukaa chini na utoro wa wanafunzi suala ambalo limetafutiwa ufumbuzi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Gaguti alisema pamoja na kero hiyo ya ukosefu wa madawati kutatuliwa Serikali imejipanga kila mwanafunzi kupata elimu bora na inayo stahili; hivyo ni jukumu la wazazi kwa kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata malezi mazuri na kuwahimiza watoto kuhudhuria shuleni ilikuweza kusoma kwa juhudi na waweze kufaulu.
Aidha Kanali Gaguti aliwataka wakuu wa shule kuweka malengo ya kupandisha ufaulu ili wilaya iweze kujipima kutoka asilimia 74.33% mwaka jana na kupanda hadi kufikia asilimia 84.3% ikiwa ndio njia sahihi ya kutathimini kama jitihada za Serikali zimefanikiwa na malengo yamefikiwa.
"Niwashukuru Wadau wote walio jitokeza kuchangia madawati katika Wilaya yetu, na Wananchi kwa kufanikisha jukumu hili. Mwitikio wenu ni ishara ya uzalendo kwa Nchi yenu na kutambua dhana ya maendeleo ya kweli ni lazima Wananchi washirikishwe. Aidha,dhana na mawazo ya Serikali kufanya kila kitu imepitwa na wakati hivyo nimefurahishwa sana na Wananchi wa Buhigwe kujitoa katika suala hili",alisema Gaguti.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga alisema wakati zoezi la utengenezaji wa madawati linaanza uhitaji ulikuwa ni madawati 18896 na madawati yaliyo kuwepo ni 7908, awamu ya kwanza yalipatikana madawati 9156 upungufu ukawa madawati 1832 siku chache zilizo pita Wilaya imekamilisha zoezi hill kwa asilimia 100% na yamekabidhiwa katika shule 88 za Wilaya hiyo.
Nyamoga aliwapongeza Wananchi pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa juhudi alizo zifanya za kuwashawishi watu na taasisi mbalimbali kichangia madawati kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha hadi sasa tatizo hilo linatatuliwa na kukamilika kwa Wakati na Wanfunzi wetu wataendelea kupata elimu nzuri .
Akisoma Risala kwa niaaba ya Wakuu wa Shule Kaimu Afisa elimu Wilaya ya Buhigwe Issa Kambi alisema katika kuunga mkono juhudi za serikali walijitahidi kuwahimiza Wananchi kuchangia madawati ambapo Wananchi walichangia madawati 430 kwa vijiji vyote na mengine kutolewa na serikali pamoja na wadau wengine na kukamilisha idadi ya madawati iliyo hitajika.
Alisema watahakikisha Miondombinu ya serikali inalindwa kwa kuweka sheria kali kwa watakao sababisha uharibifu na kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria ili kupunguza utoro na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wote.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment