NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
WANAKIJIJI
wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia
ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga
kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi
kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi.
Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.
Bi
Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa
ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.
“Nia
ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia
wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema.
Alisema,
kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme,
TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa
Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone
kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei
nafuu.” Aliongeza. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga
hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya
wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.
Akizungumzia
kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia
za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza
umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar
Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa
Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga
kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa
kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.
Mradi
huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa
na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu
shilingi Trilioni 1.
Kazi
iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba
nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba
nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika
chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme,
vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na
Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua.
Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar
Kanyama, akizungumza kwenye kituo cha Kibaoni Singida
Mkuu wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kibaoni mkoani Singida, akitoa maelezo kwa wahariri
Mhariri wa Star TV, Jenifer Sumi
Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akinakili maelezo ya kiufundi kuhusiana na kituo cha umeme cha Kibaoni mkoani Singida.
Picha ya pamoja ya wahariri na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Sinfida
Kituo cha Kibaoni mkoani Singida ambacho kilifanyiwa upanuzi chini ya mradi wa Backbone
Mdhibiti mifumo ya umeme kituo cha Kibaoni Mkoani Singida, aimuonyesha kitu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), Neville Meena
Minara ya kubeba nyaya za kusafirisha umeme, upande wa kulia ni minara mipya na kushoto ni ile ya zamani
0 comments:
Post a Comment