Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis Mwakapalila katikati wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wa kwana kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof. Isaya Jairo.
Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis.katika waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa uwasilishaji bora wa mapato wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.Na Ally Daud-MAELEZO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma zilizoandaliwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015.
Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.
Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi kwa ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.
Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi (Tanga Cement Plc) wakiibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo .
0 comments:
Post a Comment