Na Father Kidevu Blog- Kigoma
JESHI la polisi Mkoani Kigoma
limefanikiwa kukamata risasi 408 za bunduki
zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa mkazi
wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa
Habari ofisini kwake jana Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP
Fredinand Mtui alisema mnamo tarehe 5Desemba majira ya 08:20 huko maeneo ya
makere Center katika kijiji cha Makere askari wakiwa doria walipokea taarifa
kutoka kwa raia wema wanao chukia uhalifu kuwa kuna mtu wana wasiwasi nae kuwa
anamzigo usio kuwa wa kawaida.
Mtui alisema Askari walianza
ufuataliaji na kufanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake
limehifashiwa kwa shughuli za kiusalama, alipo fanyiwa upekuzi mtuhumiwa
huyokatika Sanduku lake alilokuwa
amebeba alikutwa akiwa na risasi 408 za bunduki aina ya SMG/SAR alizokuwa amezifunga ndani ya nguo zake .
Aidha Mtui alisema upelelezi
bado unaendelea ,Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria
pindi upelelezi utakapo kamilika
ilikutoa fundiaho kwa wananchi wengine wanao nunua siraha kwa lengo la
kufanyia uhalifu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
"nichukue fursa hii
kuwaasa wahalifu wanao jihusisha na biashara ya kuuza na kununua risasi na
siraha nyingine waache biashara hiyo, wafanye kazi nyingine ambazo
zinatambulika kisheria vyombo vya ulinzi na usalama viko imara kuwatafuta
wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria,"alisema Mtui.
Sambamba na tukio hilo alisema
mnamo tarehe 6Desemba huko maeneo ya Mwanga Vamia Manispaa ya Kigoma ujiji
Hussen Athuman (36) Mkazi wa mwanga Vamia alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani.
Mtui alisema usiku wa tarehe5
marehemu alimpigia simu Dada yake na
kudai kuwa walikuwa na ugomvi na mkewe
ugomvi huo uliopelekea mkewe kuondoka
siku nne zilizo pita , na kumwambia amueleze kaka yake kwamba atachukua
maamuzi magumu.
Alisema chanzo cha kujinyonga
ni ugomvi baina ya baina ya marehemu na mkewe, mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika Hospital ya rufaa maweni kusubili
kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
0 comments:
Post a Comment