Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa akiwa na tuzo waliyoshinda.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta
ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa
za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.
DCB COMMERCIAL BANK YAIBUKA MSHINDI WA
KWANZA KWA SEKTA YA BENKI, NDOGO NA KATI KWA UBORA WA UANDAAJI NA UWASILISHAJI
WA TAARIFA ZA HESABU MWAKA
2015.
Ndugu Wanahabari,
Napenda
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha hapa leo. Lengo la kuwaiteni ni
kutoa taarifa kwa umma juu ya DCB Commercial Bank kuwa mshindi wa kwanza kwa
sekta za benki, ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu mwaka 2015. Hii ni tuzo ambayo
inaandaliwa kila mwaka na Bodi ya Uhasibu Tanzania ( NBAA).
Mashindano
haya yalianza tangu miaka ya 2011, na katika kipindi chote hicho DCB Commercial
bank imeweza kufanya vizuri. Kwa miaka minne mfululizo mwaka 2011 hadi 2014,
Benki imeshika nafasi ya 3 miongoni mwa benki za Tanzania kwa ubora wa uandaaji
na uwasilishaji wa taarifa za Hesabu na kwa mwaka wa 2015, DCB imekuwa mshindi
wa kwanza kwa sekta ya benki, ndogo na za kati. Kwetu sisi ni fahari kubwa na tunajivunia
mafanikio tuliyopata ikiwa ni kielelezo kwamba DCB Benki inafuata miongozo ya
utawala bora, tunaomba wadau na wawekezaji wetu kuwa na imani juu ya usalama wa
fedha zao walizowekeza DCB. Tunawaomba muendelee kuitumia Benki ya DCB kwa
shughuli zote za kibenki. Tunaahidi kuendeleza mafanikio haya kwa ustawi wa
Benki, wateja, wawekezaji na Taifa kwa ujumla.
Ndugu Wanahabari
Mafanikio
mengine ambayo benki imepata ni pamoja na:-
· Kutimiza miaka 14 ya utoaji huduma bora za
kibenki kwa Wajasiriamali, mwaka 2017 benki itasheherekea miaka 15 ya utoaji
huduma bora kwa wajasirimali.
· Benki imepata faida kila mwaka kuanzia mwaka 2006
· Kulipa gawio kwa wanahisa wa benki kila
mwaka
· Kuongezeka kwa matawi kutoka matawi 2 mwaka
2005 hadi matawi 9 mwaka 2016. Mwaka 2017 benki itafungua tawi la 10 makao
makuu ya nchi, Dodoma.
·
Kuwa na mtaji imara wa shi. Bilioni 32.
· Upanuaji na uboreshaji wa huduma za kisasa
kwa wateja wetu kupitia Agency Banking (DCB Jirani) ambayo inawawezesha wateja
wetu kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala walioidhinishwa na
DCB katika vitongoji, DCB Pesa huduma ambayo inamuwezesha mteja kufanya miamala
ya benki kutuma na kupokea pesa kupitia simu ya mkononi, kupata huduma hii si
lazima mteja kuwa na akaunti na DCB Benki. Huduma hii ni mpya, pamoja na agency
Banking zitazinduliwa rasmi Januari mwakani, leo tumewaita mawakala wetu
kuongea nao juu ya kuanza kipindi cha majaribio cha mwezi na baada ya
kujiridhisha tutazindua rasmi huduma hizi.
Ndugu Wanahabari
Kwa
sasa benki iko kwenye promosheni ya Boresha maisha na DCB, pata faida na DCB ya
hadi asilimia 15% kwa kufungua akaunti ya amana za muda maalum. Tunatoa wito kwa wateja wetu na wasiowateja,
mashirika ya umma, wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kufungua akaunti au
kuweka pesa kwenye akaunti ili muweze kujipatia zawadi mbalimbali baada ya
kushinda bahati nasibu.
Mwisho
Uongozi
wa benki unapenda kuwatakia wateja wake na wananchi kwa ujumla sikukuu njema ya
Christmas na mwaka mpya 2017.
E.P.
MKWAWA
MKURUGENZI
MTENDAJI
DCB
COMMERCIAL BANK PLC
DISEMBA
2016.
0 comments:
Post a Comment