Na Bety Alex, FK Blog-Arusha
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,
Alexander Mnyeti, ameagiza wenyeviti wa vijiji katika Wilaya hiyo
kuwapa adhabu kali baadhi ya wazazi na walezi ambao watabainika kuingia
kwenye majumbaa ya starehe na pombe wakiwa wameambatana na watoto wao.
Hataivyo adhabu hizo ni pamoja na kuwatandika viboko hadharani wazazi hao kwa kuwa hawawajengi watoto vema
Aliyasema hayo wiki iloyopita wakati akiongea na wenyeviti wa vijiji kutoka katika vijiji vyote vya wilaya hizo.
Aidha mnyeti alifafanua kuwa haipendezi hata kidogo kwa
baadhi ya wazazi kujisahau suala zima la malezi hadi wafikie hatua ya
kutaka kwenda kwenye majumba ya starehe na watoto
Aliongeza hiyo ni tabia ya kupingwa na kukataliwa kabisa na
wadau pamoja na uongozi wa kata na endapo watakapombaini muhusika basi
wanatakiwa kumpa adhabu Kali.
"Nimewapa mamlaka kabisa ya kuwachapa viboko ambao
watabainika kufanya hivi na mkifanya hivi itawajengea jamii tabia
nzuri'aliongeza Mnyeti.
Wakati huo huo aliwataka wenyeviti pamoja na watendaji pia
kuwapa adhabi kali baadhi ya vijana ambao watajihusisha na unywaji wa
pombe za kawaida na haramu wakati wa kazi.
Alibainisha kuwa unywaji wa pombe wakati wa kazi sio tendo
zuri hata kidogo na kwa hali hiyo pia mnatakiwa kutoa adhabu kali kwa
wote watakaokutwa 'Hakikisheni kuwa mnawatandika ipasavyo wote ambao
watakutwa na kosa hili kwani ninyi mna uwezo mkubwa wa kutengeneza hii
jamii'aliongeza Mnyeti
Akiongea kwa niaba ya wenyeviti mmoja wa wenyeviti hao,Luca
Daniel alisema kuwa wananchi wanapaswa kutii mamlaka ambazo zipo na
kama watafanya hivyo wataweza kuruhusu amani kuwa ya kudumu.
0 comments:
Post a Comment