Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiwa katika mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi.
Mwalimu wa Chuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunnzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.
*****************
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka
ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi
inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha
watanzania tamaduni ,mila na desturi ili kuulinda utamaduni wetu ambao
unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza
na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu
wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania .
Amesema
utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya
utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi
duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema chuo VETA Mikumi kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Communinity College cha nchini Canada kinaanda kozi hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali.
Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
Aidha
mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo
wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia
technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala.
Ayo
amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka
katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa
na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa
rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro
kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa
sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na
serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka
msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda.
0 comments:
Post a Comment