Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem
Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo
alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na
kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia
ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter
Kisenge.
*****************
Na Anna Nkinda - JKCI
SERIKALI ya
Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vifaa
vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine na vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika
katika chumba cha upasuaji.
Ahadi hiyo imetolewa leo
na Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem
Al Najem
alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya
kuangalia ni jinsi gani nchi yake
inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa
tiba.
Mhe. Balozi Al Najem alisema
vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu vitapatikana kabla ya
kumalizika kwa mwaka huu ambapo vifaa pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana
mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017.
“Serikali ya nchi yangu
inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii pamoja na Taasisi zingine
zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini ili watanzania waweze
kupata huduma bora”, alisema Mhe. Balozi Al Najem.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
Prof. Mohamed Janabi alishukuru Serikali
ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na mashine zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa
moyo.
“Tuna vyumba vitatu vya
upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina vifaa, kupatikana kwa
vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait kutatufanya tuwe na vyumba vya
upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia kutoa
huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .
Akiwa katika Taasisi hiyo
Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa
walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa.
0 comments:
Post a Comment