Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akimkabidhi
Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akimkabidhi
Bendera ya Taifa Julietha Kabete (kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati
wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa mrembo Julietha Kabete atakayeiwakilisha
Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania. Kutoka Kulia ni Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye, Katibu wa Kamati, Bosco Majaliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Internationa Agency, Hasim Lundenga.
************
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika
mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika
mashindano hayo.
Nape ametoa ahadi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la
Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Nnauye ameongeza kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija kwa Taifa hasa katika
kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili
linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa
mashindano ya urembo nchini” alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese
group Ltd,Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea
sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo
kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“ kwa niaba ya Millen Magese
group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania kwa kutuunga
mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika mashindano haya”Alisema Chuma.
Kwa upande wake Mshiriki kutoka
Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete ameishukuru
Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi kuitangaza nchi yangu
vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na wanipigie kura
ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika urembo” Alisema
Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika
yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross
River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza
na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment