Nafasi Ya Matangazo

November 28, 2016

Na Bety Alex,Arusha
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto Ramadhani Idi mwanafunzi wa darasa la sita kutoka katika Shule ya Msingi ya Albeije Francosea, amemuomba Raisi  John Pombe Magufuli kumsaidia apate mikono ya bandia ili aweze kutimiza ndoto zake za masomo.

Aidha mtoto huyo ambaye ni mlemavu wa mikono amedai kuwa ili kufanikisha zoezi hilo kunaitajika kiasi cha milioni kumi.

Akiongea juzi kwenye maafali ya sita ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo mwanafunzi huyo alisema kuwa kwa kuwa raisi magufuli anasisitiza elimu bora ni muimu sana akaweza kumuangalia hata na yeye.



Ramadhani alisema kuwa kwa sasa anapata shida kubwa sana ya kuweza kuandika kwani anatumia miguu kwa ajili ya kuandika lakini kama akipata mikono ya bandia itamsaidia kuandika lakini hata kufanya kazi nyingine za shule kwa kutumia mikono.

"Mimi namuomba raisi magufuli aweze kuniona katika hali yangu lakini pia hata wasamaria wema wengine kwani Nina ndoto za kuja kuwa rubani"aliongeza Ramadhani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Awali Meneja wa shule hiyo bi Hindu Ally alisema kuwa mwanafunzi huyo anahitaji msaada mkubwa na jamii inatakiwa iweze kumsaidia kwa kuwa mpaka sasa ameonesha moyo wa masomo.

'Tukiangalia ripoti za mwanafunzi huyu kwa kweli zinaridhisha sana akifeli sana unakuta kashika nafasi ya tatu na hapo ana mikono anatumia miguu yake kuandika na ana ndoto za kuwa rubani"aliongeza Hindu.

Hataivyo kwa upande wa baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Idi Rashidi alisema kuwa wameshafanya mikakati mbalimbali ya kuweza kumsaidia mwanafunzi huyo lakini wameambiwa na madaktari bingwa kuwa msaada wa kuweza kupata mikono ya bandia upo nchini Canada.

Idi alisema kutokana na hali ya maisha wameshindwa kutimiza hilo ingawaje mtoto ana moyo wa kupenda na kujali masomo sana.
Posted by MROKI On Monday, November 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo