Ilhan Omar, mwenye umri wa
miaka 34, ameweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomalia
nchini Marekani.
Mwanamke huyo Muislamu mwenye
asili ya Somali na Marekani ndio raia wa kwanza wa Kisomali kuchaguliwa katika
wadhfa mkuu kama huo nchini Marekani.
Uchaguzi wake unajiri siku
chache tu baada ya rais mteule Donald Trump kushtumu wahamiaji wa Kisomali
mjini Minnesota kwa kueneza maoni ya itikadi kali.
Akisherehekea ushindi wake bi
Omar amesema kuwa atakuwa sauti ya waliotengwa katika bunge la jimbo hilo.
''Nadhani nimeleta sauti ya
akina mama vijana wanaotafuta fursa''.
Redio ya uma katika jimbo hilo
ilimnukuu akisema kuwa alitoroka nchini Somalia na familia yake wakati wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe wakati alipokuwa na umri wa miaka minane pekee.
Waliishi nchini Kenya kama
wakimbizi kwa takriban miaka minne kabla ya kuelekea Marekani na kuishi katika
jimbo lenye Wasomalia wengi la Minnesota. Source: BBC
0 comments:
Post a Comment