Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar (CCM), Hafidh Ali Tahir amefariki dunia.
Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilila ameiambia Habarileo Online asubuhi hii kuwa Tahir alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo japo si kwa kiwango kikubwa na alikuwa akipata matibabu na kuebndelea na shughuli zake lakini jana majira ya saa 8 usiku alizidiwa na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na baadae saa 9 alfajiri ya kuamkia leo alifikwa na umauti.
Dk Kashilila alisema hadi jana jioni alikuwepo Bungeni.
Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.
Marehemu pia alikuwa mwamuzi wa FIFA na mwana-Yanga kindakindaki na ni jana tu amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge wanaYanga mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto.
Taarifa kamili itatolewa hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment