Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara
kiwandani hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa Makamu wa
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan juu ya
maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara
wazawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula ,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.
****************
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali
inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama
hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa
watanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya
kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili
kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia
kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Makamu wa
Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina
uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka
utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero
kwenye viwanda.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi vinajengwa
nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini hali ambayo
itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kuuzwa kwenye masoko ya
nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na kuongeza ajira kwa makundi
mbalimbali ya wananchi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda mkoani
Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za uzalishaji na pale
kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia
kazi na Serikali.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal amesema
kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye Viwanda
hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi
kwa Watanzania.
Amesema kwa
sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa Tanzania
pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika maeneo
mbalimbali nchini.
0 comments:
Post a Comment