Nafasi Ya Matangazo

October 11, 2016

 Mkuu wa Wilayaya Same, mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemare Staki Senyamule, (kulia), akimkaribisha ofisini kwake, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele Oktoba 10, 2016
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SAME
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Staki Semanyule, (pichani), amesema wilaya yake inazo fursa za kutosha hususan kilimo cha Tangawizi na kuukaribisha Mfuko wa Pensheni wa PPF kujenga kiwanda cha kuchakata Tangawizi, ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo katika mazungumzo mafupi na MenejaUhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele, aliyemtembelea ofisini kwake Oktoba 10, 2016.

“Same tunalima Tangawizi kwa wingi, wakulima hawapati faida ya kutosha kwa vile wanauza mara tu wanapovuna, tunahitaji viwanda vya kuchakata Tangawizi ili iwe katika mfumo wa unga (powder) na itakuwa rahisi kusafirisha nje na kuuza kwa bei ya juu zaidi na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima wetu.” Alisema Bi Staki.

Bi. Staki pia alisema, ukiacha wananchikujishughulisha na zao hilo, pia Same wanalima mazao ya chakula kwa wingi.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, PPF inaendelea na kampeni yake ya kuongeza wanachama hususan kupitia mpango wa “Wote Scheme” unamuwezesha Mfanyakazi wa sekta rasmi na isiyo rasmi, (wajasiruimali) kujiunga nao.

“ Wote Scheme, ni mpango utakaowafaa sana wajasiriamali, ambao ni wakulima, waendesha bodaboda, mama lishe na baba lishe.” Alisema Bi Mengele.

Akifafanua zaidi, Bi.Mengele alisema, Mwanachamaaliyejiunga na mpango huo, atafaidika na Mafao mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata Bima ya Afya.
 Bi. Staki akimsikiliza Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
Meneja Uhusiano wa PPF, Bu.Lulu Mengele, (kushoto), akimueleza Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemary Staki Semanyule, shughuli mbalimbali zifanywazo na PPF hususanMpango wa Wote Scheme.
Posted by MROKI On Tuesday, October 11, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo