Nafasi Ya Matangazo

October 09, 2016

 Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyagi, Devis Deogratius (wa pili kutoka kulia) akimpongeza mfanyabiashara wa kampuni ya Stewart Jacob Ulomi, Grace Oroki baada ya kuibuka mshindi wa  gari lenye thamani ya Sh56 milioni kutoka kampuni ya hiyo katika mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni  hiyo.

Mshindi wa Promosheni ya konyagi akiwasha gari alilojishindia
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyagi, Devis Deogratius (wa pili kutoka kulia) akikabidhi  katoni ya Konyagi mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya mchezo wa bahati nasibu uliochezeshwa na kampuni hiyo
**************
MFANYABIASHARA kutoka kampuni ya Stewart Jacob Ulomi, Grace Oroki, mkazi wa Jijini Dar es salaam, ameibuka mshindi wa gari lenye thamani ya Sh56 milioni katika mchezo wa bahati nasibu ya kwanza ya promosheni ya nunua ,uza ,shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya TDL. 

Droo ya kwanza yapromosheni hiyo ilifanyika katika viwanja vya hoteli ya New City Pub jijini Mbeya na ulikuwa na washiriki 25 chini ya usimamizi wa Ofisa Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha , Abdalah Abeid,na ilikuwa kwa ajili ya mawakala Konyagi kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Pwani. 

Akiongea kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Oriki alisema hakutegemea kama angeweza kupata gari hilo kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo na amepata faraja kwa kuweza kuibuka mshindi. “Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona.Sikutegemea kuwa nitaibuka na ushindi, ikizingitia awali wote tulikosa ikalazimika kufanya droo mwa mara ya pili na Mola ameniona kuwa mimi ndie mwenye bahati hiyo. Ni mchezo mzuri uliokuwa wa wazi kabisa. 

"Na gari hili litanisaidia sana kukuza kupato changu katika biashara ya kusambaza bidhaa za kampuni ya konyagi kwa wateja wangu,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Konyagi, Devis Deogratius.

Alisema lengo la mchezo huo kwa wateja wake ni kuona anayebahatika anakuwa na uwezo wa kujiongeza katika biashara yake ya usambazaji bidhaa za Konyagi. 

Alisema mchakato wa kuwapata washiriki ulianza Julai mwaka huu na umechukuwa muda wa miezi mitatu hadi kukamilika na wafanyabiashara (washiriki) waliingia kwenye droo hiyo baada ya kujiridhisha kwamba kila mmoja ametimiza masharti na vigezo vilivyowekwa na kampuni hiyo. 

Alisema mbali na mshindi huyo wa gari katika droo hii ya kwanza washiriki watano walibahatika kujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja. Baadhi ya washiriki katika droo hiyo, Augustine Kisinga na Sebastian Kavishe walisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.

Kisinga alisema ‘Kwanza Konyagi kupitia mchezo wa bahati nasibu umetukutanisha na wanafanyabiashara wa maeneo mengine, kwa mfano mimi hapa nilikuwa sijawahi fika Mbeya lakini leo hii nimefika na nimeifahamu Mbeya. 

Kwa upande wake, Sebastian Kavishe aliishauri kampuni hiyo kufanya Promosheni kama hizo mara kwa mara ili kuwapatia motisha wasambazaji wao wakubwa na kuongeza kuwa zawadi kwa washindi sio lazima ziwe kubwa kama gari bali zinaweza kutolewa zawadi ndogo kama Pikipiki au Bajaj ili kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa na nafasi ya kushinda na kupata nyenzo za kuwasaidia katika biashara zao. 
Posted by MROKI On Sunday, October 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo