Nafasi Ya Matangazo

October 25, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizindua rasmi ujenzi wa vyumba vya madarasa 176 Wilayani humo.
Kanali Marco Gaguti akizungumza jambo na viongozi Wilayani humo.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti amezindua ujenzi wa madarasa 176 ya shule za  msingi Wilayani Buhigwe ilikuhakikisha wanamaliza kero ya upungufu wa madarasa katika wilaya hiyo ambayo yatakamilika kwa Kipindi cha Mwaka mmoja ili kumaliza kero ya muda mrefu. 

Akizungumza na  Wananchi wa wilaya Hiyo katika uzinduzi wa Ujenzi wa Vyumba vya madarasa  katika kijiji cha Mnyegera aliwaomba Wananchi Kumuunga mkono ilikuhakikisha Wanamaliza tatizo hilo na watoto wanasoma Katika Mazingira mazuri na kupata elimu nzuri itakayo wasaidia kuepukana na umasikini.


Gaguti alisema Baada ya kuona hali ya ukosefu wa madarasa katika Wilaya hiyo inayopelekea Wanafunzi kukosa vyumba vya kusomea kutokana na wingi wao aliamua kuweka kambi katika kila Kata kujenga shule mbili ambapo anatarajia kujenga shule 176 kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo ilikuepukana na upungufu wa Vyumba vya madarasa.

" Baada ya kuona takwimu na kujionea hali halisi ya Shule Zetu nilitambua nilazima tuchukue Jukumu la kubadili hali hii nitaweka Kambi Kila Kata kuhakikisha Jukumu hili linakamilishwa Ndani ya Muda tuliojipangia,pia ni washukuru Wananchi na viongozi kwa muitikikio na Dhamira ya kushirikiana na Serikali kuboresha miundo mbinu ya Elimu",alisema Gaguti.

Nae Afisa Elimu wa Halmashauri ya Buhigwe ,Deo Fande  alisema Halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa Vyumba vya Madarasa 672 kutoka na Elimu kutolewa bute wazazi wengi wameleta watoto wao iliwaweze kupata elimu hiyo hali iliyo pelekea upungufu wa madarasa.

Fande alimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutoa kipaumbele cha kujenga madarasa na aliwaomba Wananchi kuendelea kujitoa kwa Wingi kuchangia kujenga madarasa yatakayo kuwa hayakujengwa na Wilaya na kushirikiana na viongozi kujenga madarasa hayo.

Kwa upande wao Wananchi Wa Wilaya ya Buhigwe ,Pelesi Makaya na Abasi Mvuyekule walisema wanampongeza Mkuu wa Wilaya kwa kujitoa kushirikiana na Wananchi kwa kuwasaidia watoto wao kuepukana na mazingira magumu ya kusomea iliyo kuwa ikiwatesa watoto hao.

Aidha Wananchi hao wamemuahidi Mkuu wa Wilaya kushirikiana nae kwa kuchangia maendeleo na kuwawezesha Watoto kukaa na kupata madarasa mazuri yatakayo pelekea watoto kupata elimu iliyo bora na itakayo wasaidia katika maisha yao.
Posted by MROKI On Tuesday, October 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo