Ma Meneja wa
viwanda vya bia vya TBL Group wakiwa wameshikilia vikombe vya tuzo ambazo
kampuni imeshinda katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam muda mfupi baada ya
kurejea kutoka nchini Afrika ya kusini
Baadhi ya
wafanyakazi wa TBL Group na ma Meneja wa viwanda vya
bia wakishangilia ushindi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es
Salaam.
Baadhi ya
wafanyakazi wa TBL Group na ma Meneja katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa
ndege wa Dar Salaam.
*********
KAMPUNI ya TBL Group imezidi kung’ara kimataifa kutokana na
viwanda vyake vya kutengeneza bia vilivyopo kwenye mikoa ya Dar es
Salaam,Mbeya,Mwanza na Arusha kushinda tuzo za juu za kimataifa za SABMiller
kwa uzalishaji bora ambapo pia bia aina ya Safari Lager imetangazwa kuwa ni bia
bora (Champion Beer) barani Afrika. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kampuni ya SABMiller imekuwa na utaratibu wa kushindanisha viwanda
vyake vilivyopo kwenye nchi mbalimbali na kutoa vigezo vya kushindania kigezo
kikubwa kimojawapo kikiwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa .
Hafla ya kutangaza viwanda vilivvoshinda na kuvipatia tuzo ijulikanao
kama SABMiller Africa Technical Awards ilifanyika jana nchini Afrika na
kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi wa kampuni hiyo wakiwemo mameneja wa viwanda
vya bia kutoka kampuni zake tanzu.
Bia aina ya Safari Lager iliyozalishwa katika viwanda vya TBL vya Dar
na Arusha ilitangazwa bia bora barani na kutunukiwa tuzo,kiwanda cha Dar
kikiwa kimeshika nafasi ya kwanza na Arusha nafasi ya pili.
Tuzo nyingine ambazo viwanda vya TBL Group vimeshinda ni tuzo ya
uzalishaji wa bia bora ya Castle inayojulikana kama.
Mick Steward Castle Lager award ambapo kiwanda cha TBL Dar es Salaam
kimeshika nafasi ya kwanza,TBL Mbeya nafasi ya pili na TBL Arusha nafasi ya
tatu.
Nyingine ni Tuzo ya Upishi Bora wa bia ya mwaka (Brewery of the Year
Award),ambapo kiwanda cha TBL Mbeya kimeshika nafasi ya kwanza na kiwanda cha
TBL Mwanza kimenyakua nafasi ya pili.Pia kampuni imeshinda tuzo ya kufuata
kanuni bora za Ununuzi na Ugavi (Supply Chain and Planning award).
Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group,Gavin Van Wijk amevipongeza viwanda
vyote kwa kuibuka na ushindi wa tuzo kubwa za SABMiller.
“Ushindani ulikuwa mkubwa ukihusisha viwanda vingine kutoka nchi
mbalimbali duniani,inafurahisha kuona viwanda vya Tanzania vinachomoza na
kushinda tuzo kama hizi,hii inadhihirisha kuwa TBL imejipanga kwenda sambamba
na mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda kwa kuwa mafanikio
haya yanaletwa na watanzania wenyewe”.Alisema.
Wijk aliwashukuru wateja wote wa bidhaa za TBL Group kwa kuiunga mkono
kampuni na aliahidi kuwa kampuni itaendelea kuzalisha bora wakati huo huo
ikishiriki kusaidia miradi mbalimbali ya kuboresha maisha ya wananchi hususani
katika sekta za kilimo,mazingira,elimu na afya.
Akiongea kwa niaba ya Mameneja wa viwanda vya TBL Group vilivyoshinda
tuzo,Meneja wa kiwanda cha Dar es Salaam,Calvin Martin amesema wamefurahishwa
kuona viwanda vya Tanzania vinafanya vizuri na kutambuliwa kimataifa “Tuzo hizi
zinatokana na mchango wa kila mfanyakazi wa kampuni,tuzidi kuongeza bidii
katika kazi tutazidi kufanya vizuri zaidi na tunashukuru wateja wetu wote kwa
kutuunga mkono kwa kutumia bidhaa zetu ,tumejipanga kuhakikisha wanazidi kupata
bidhaa zetu kwa ubora mkubwa na kwa urahisi popote walipo”.Alisema Calvin.
Wakati huohuo,Mhandisi wa kitanzania,Richmond Raymond ,ambaye alikuwa
ni Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Mwanza kwa sasa hivi akiwa amehamishiwa nchini
Afrika ya kusini kuwa Meneja wa Kiwanda cha bia cha Polokwane kilichopo
nchini Afrika ya Kusini ametunukiwa tuzo maalumu ya kutoa mchango mkubwa kwa
kampuni inaojulikana kama SABMiller Brewery Legend status katika hafla
hiyo.
0 comments:
Post a Comment