Afisa mawasiliano ya mambo ya nje wa TBL Group,
Amanda Walter, akipokea cheti cha uchangiaji wa shughuli za wiki ya Usalama
Barabarani kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani,
Hamad Masauni,kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya Nenda kwa usalama barabarani
iliyofanyika mkoani Geita.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi kutoka Kitengo
cha Usalama barabarani cha Jeshi la Polisi.
***************
KAMPUNI ya TBL Group imetunukiwa cheti kutokana
na mchango wake mkubwa katika kuendesha kampeni za Usalama barabarani nchini
ikiwemo kudhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani mwaka huu ambayo
imezinduliwa kitaifa mkoani Geita.
Cheti hicho kutoka serikali kilitolewa na Naibu
wa Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
hafla hiyo iliyojumuisha viongozi na watumishi wa serikali wakiwemo wawakilishi
kutoka makampuni na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akiongea baada ya hafla hiyo,Afisa Mawasiliano
ya Nje wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa TBL Group imekuwa mstari wa
mbele kuendesha kampeni za Usalama Barabarani na kudhamini Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani na itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine
katika kufanikisha kampeni hizi kwa lengo la kupunguza matukio ya ajali nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Mwaka huu mbali na kutoa stika na vifaa
vingine vya uhamasishaji tunalo gari maalumu la kupima afya za madereva bure
ambalo liko hapa Geita na litaendelea kuzunguka sehemu mbalimbali nchini kwa
ajili ya kutoa huduma hiyo.Natoa wito kwa madereva kujitokeza kupima afya zao
na kupatiwa matibabu”.Alisema Walter.
Aliongeza kuwa mbali na kupima afya za madereva
kampuni imeandaa mafunzo mbalimbali endelevu kwa ajili ya masuala ya usalama
kwa wafanyakazi wake na makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo
mafunzo ya kuhamasisha unywaji kistaarabu lengo kubwa likiwa ni kuleta
mabadiliko kwa watumiaji wanaotumia vinywaji vyenye kilevi wasiathirike
kwa kutumia vinywaji na kuleta athari nyinginezo zitokanazo na ulevi kama vile
ajali za barabarani.
Amanda pia alisema kuwa kampuni kutokana na
kutekeleza na kuzingatia kanuni za usalama hivi karibuni ilishinda tuzo
mbalimbali za usalama moja wapo ikiwa tuzo ya usalama sehemu za kazi inaotolewa
na taasisi ya OSHA ambapo pia ilishinda tuzo a kimataifa ya Usalama ijulikanayo
kama NOSA.
Wakati huohuo, gari la kupima afya za madereva
la zahanati mwendo limekuwa moja ya kivutio kikubwa katika uzinduzi wa kampeni
za Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambapo madereva wengi na wananchi
walijitokeza kwa ajili ya kupima afya zao na kupatiwa matibabu.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye uwanja wa
Geita na kushuhudia huduma za upimaji wa afya kwa madereva wameipongeza TBL
Group kwa kuanzisha huduma hii ambayo itawawezesha madereve wengi kupima afya
zao “Unajua madereva tumekuwa hatuna muda wa kwenda katika vituo vya afya
kupima afya ila kwa njia hii ya basi linalotembea tutafikiwa wengi”.Alisema
Josephat Ngosha dereva wa malori na mkazi wa Geita mjini.
0 comments:
Post a Comment