Mkuu wa Wi;laya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Marco Gaguti.
Na Mwandishi wetu, Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Col
Marco Gaguti amewaonya watendaji wa Wilaya ya Buhigwe kuepuka kuwa chanzo cha
migogoro ya Wananchi kwa kukwamisha shughuli za maendeleo ya
Wananchi na kulinda maslahi yao binafsi na kushindwa kuwatumikia
Wananchi ipasavyo.
Wito huo aliutoa jana katika
Mkutano wa hadhara uliofanika katika viwanja vya shule
ya msingi Buhigwe wakati akipokea malalamiko ya Wa nanchi wa vijiji
vya Buhigwe na mlela aliwaomba watendaji kutatua kero hizona kuacha tabia ya
kuchochea migogoro ya Wananchi.
Gaguti aliwataka
Watendaji kuwahudumia Wananchi kwa haraka na kutatua kero mbalimbali
zinazo wakabili ili kupunguza migogoro na kuepuka kua chanzo cha migogoro kwa
Wananchi kwakuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali inayo wahudumia wananchi
na sio Serikali inayo jail maslahi ya mtu binafsi.
“kiongozi ambaye amekuwa
chanzo cha migogoro badala ya kuwa njia ya kutatia
migogoro hiyo na kiongozi ambaye hashughulikii matatizo ya Wananchi
kwa wakati hatufai wale ambao wapo chini ya mamlaka yangu tukiwabaini tutawachukulia
hatua za kisheria, na kwa wale mlio wachagua na hawaendani
na na malengo mlio jiwekea watoeni taratibu zipo wazi”,alisema
Mkuu wa Wilaya. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Hata hivyo katika mkutano huo
Gaguti aliwaomba Wananchi kuendelea kudumisha amani kwa kushirikiana na vyombo
vya dola katika kuwabaini watu wenye nia mbaya na wahamiaji
haramuambao baadhi yao wamekuwa chanzo cha uhalifu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata
ya Buhigwe Venas Kigwinya alisema kumekuwa na malala miko
mengi kutoka kwa Wananchi kutoka katika kijiji cha mlela waki mtuhumu mendaji
wa kijiji katika suala la maji kuwa fedha zinazo kusanywa kwenye vyanzo vya
maji hazijulikani zina kwenda wapi na kwenye mikutano ya kijiji
Wananchi hawasomewi mapato na matumizi yatokanayo na makusanyo ya fedha za
maji.
Kigwinya alisema eneo linguine
la migogoro inyo sababishwa na watendaji ni suala la uuzaji wa viwanja bila
kufuata utaratibu na wa uuzaji wa viwanja hivyo, na suala lingine ni uuzaji wa
misitu ya kijiji kwa kutoa taarifa za uongo na kero hizo alizitatulia ufumbuzi
ikiwa ni pamoja na kwenda kumomba Mkurugenzi kumuondoa mtendaji huyo na
kuwaletea Mtendaji anae jali maslahi ya Wananchi.
Kwa upande wao Wananchi
wa Kijiji cha Mlela ,Festo Nyamunda na Rejina Laurenti walisema kumekuwa na
kero ya viwanja kuuzwa na mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji bila
kufuata utaratibu wa kuwashilikisha Wananchi suala linalo pelekea migogoro kwa
Wananchi, mpaka sasa katika kijiji hicho hakuna maeneo yaliyo
tengwa kwaajili ya huduma za kijamii kama Shule na vtuo vya Afya ili
kuwasaidia Wananchi hao.
Walisema kunatatizo
lilijitokeza katika Kijiji hicho cha Mwenyekiti wa kijiji na Mtendaji waliuza
msitu miti 200 na kuwadanganya Wananchi miti iliyo uzwa ni miti 15, na sisi
tunaona miti inaendelea kukatwa hiyo ni moja ya sababu inayo weza kupelekea migogoro
baina yetu wana kijiji na wawekezaji inayo sababishwa na watendaji hao.
0 comments:
Post a Comment