Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili
katika eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.
Kivuko cha Pangani II pamoja na kivuko kipya MV. Tanga vikiwasili katika
eneo la Pangani Jijini Tanga.
Abiria na Magari yakiteremka kwenye kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa
huduma eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.
**************
Na Theresia Mwami TEMESA
Wananchi wa Pangani na Bweni
mkoani Tanga wamepata kivuko kipya cha MV. Tanga, ambacho sasa kitasaidiana na
MV. Pangani II kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni.
Akiongea na wananchi wa
Pangani Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase amesema kukamilika
kwa ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Tanga ni muendelezo wa sera ya Serikali ya
kuboresha huduma ya vivuko katika maeneo mbalimbali yaliyo na mahitaji ya
vivuko nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“TEMESA imejipanga kuhakikisha
kuwa vivuko vyake vyote vinafanyiwa matengenezo ya kinga kwa wakati, ili
kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi wanaotumia vivuko hivyo inapatikana kwa
wakati muafaka” Alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi Manase ameongeza kuwa
hivi sasa MV. Pangani II itakwenda kwenye ukarabati mdogo na baada ya
ukarabati huo vivuko vyote viwili vitabakia katika eneo la Pangani na Bweni ili
kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Lazaro Vazuri alisema kuwa kivuko cha MV. Tanga ni mwanzo wa uboreshajji wa huduma
ya vivuko nchini na kwa sasa wapo katika mikakati ya kukarabati vivuko vilivyopo
na kujenga vivuko vibya ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vivuko
katika maeneo yenye huhitaji.
Mmoja ya wananchi wa Wananchi
wa Pangani/Bweni Bw. Othman Juma Ali ameipongeza Serikali kwa juhudi za
kupambana na changamoto ya vivuko inayozikumba sehemu nyingi zilizozungukwa na
maji.
“Tumekipokea kivuko cha MV.
Tanga kwa furaha kubwa na tunaiomba Serikali kutoa huduma ya kivuko hiki kwa
saa 24 kila siku ili kitusaidie wananchi hasa wa eneo la Bweni kupata
huduma hiyo nyakati za usiku tunapohitaji kupata huduma za kijamii upande wa
Pangani” alisema Bw. Othman.
MV. Tanga imesanifiwa na
kutengenezwa na Kampuni ya kitanzania ya Songoro Marine Company Ltd na kivuko
hiki kina uwezo wa kubeba tani 50 ambazo ni sawa na kubeba abiria 100 na magari
6 kwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment