Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamis Kigwangalla akiwasili katika ofisi za kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiandika maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha wakati alipotembelea katika kituo hicho chenye maskani yake Upanga, Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 15.2016
Mkurugenzi wa kituo COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA) Bw. John Kashiha akielezea miradi mbalimbali ya kituo hicho kwa Naibu Waziri. (Hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA). BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu akiwa pamojana wasaidizi wake wakifanya upekuzi katika ofisi za kituo hicho cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA), Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla.
Upelelezi na Upekuzi ukiendelea ndani ya kituo hicho...
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo na kuwaonyesha moja ya makablasha (file) zilizokutwa hapo ilikusadia uchunguzi kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimweleza jambo Bwana John Kashiha wakati wa tukio hilo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya nyaraka za taasisi za kituo hicho
Upekuzi ukiendelea..Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha moja ya kijarida kwa Mkuu wa upepelezi wa Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY-(CHESA)
Upekuzi ukiendelea.. katika ofisi hizo.
*********
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha
COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo
Upanga, Wilayani Ilala, jijini Dar es salaam.
Ziara
hiyo ya kushtukiza inafuatia baada ya hatua ya Naibu Waziri huyo wa
Afya Dk.Kigwangalla kuendelea kufanya ukaguzi wa Asasi mbalimbali
zisizo za kiserikali zikiwemo NGO’s na CBO zenye makosa ya kiutendaji na
kimfumo ambayo ni tofauti na taarifa zao katika usajili wa Serikalini
na namna ya uendeshaji wa wao.
Mbali
na hayo kituo hicho cha CHESA kinashukiwa kuhusika na vitendo vya
uhamasishaji wa mahusiano ya mapenzi ya Jinsia moja (USHOGA), ambayo ni
kinyume na mila na Desturi za kitanzania pamoja na Katiba na sharia za
Nchi.
“Mahusiano
ya jinsia moja si kinyume na mila na desturi zetu tu. Bali hata sheria
na katiba ya nchi yetu haziruhusu mfumo huo wa kimahusiano” amesema
Dk..Kigwangalla
Aliendelea
kubainisha kuwa : “Sisi kama Serikali hatujawahi kusaini mikataba
yoyote ya kimataifa inayoruhusu ushoga hivyo kwa taasisi yoyote hapa
Nchini inayofanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi na inapaswa
kuchukuliwa hatua kali za kisheria na hata kufutiwa usajili wake”
aliongeza Dk. Kigwangalla.
Katika
ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa
ameambatana na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara
anayoiongoza, Bw. Julius Mbilinyi pamoja na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Ilala, Hassan Selengu pia wamefanya ukaguzi katika kituo hicho ili
kubaini kama kuna uwepo wa vilainishi vinavyotumiwa na watu wenye
mahusiano ya jinsia moja ambavyo hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku
matumizi yake hapa nchini.
“Serikali
ilikifuta kituo cha ‘SISI KWA SISI’ kwa sababu kilihusika na tuhuma za
ushawishi wa mahusiano ya jinsia moja ambacho pia wewe ulikuwa
Mkurugenzi wake. Sasa tumeamua kuchunguza na kituo hichi ili tujue kama
mnahusika na vitendo hivyo ili tuchukue hatua endapo itabainika ama la”
ameeleza Dk. Kigwangalla.
Aidha,
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amemtaka Mkuu wa upepelezi Bwana
Hassan Selengu afanye uchunguzi wa kina katika kituo hicho ili kubaini
pesa za misaada katika kituo hicho zinatokea wapi lakini pia ni kubaini
kama kituo hicho kinajihusisha na ushawishi wa watu kujiunga na
mahusiano ya jinsia moja.
“Tunawasiwasi
kuwa mnapokea pesa nyingi na misaada mingi kutoka katika Taasisi
mbalimbali lakini pesa hizo zinatumika kuhamasisha mapenzi na mahusiano
ya jinsia moja.
Mbali
na hayo. taarifa za usajili wa kituo hichi zinakinzana na malengo na
miradi inayofanyika hapa. Pia ipo miradi mbalimbali ambayo
haijasajiliwa wala hujaitaja katika maelezo yako lakini inafanyika
katika kituo hichi” alihoji Dk. Kigwangalla huku akimtajia baadhi ya
miradi hiyo ambayo Serikali inaitambua.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Tazama hapa MO TV, kuona tukio hilo:
0 comments:
Post a Comment