Mkurugenzi wa Mauzo na Usamabazaji wa TBL Group Gareth Jones
(Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kampuni ya Kupata kuna Mungu ya
Kijichi jijini Dar Es Salaam, Jimson Sunzu Ufunguo wa pikipiki ya
matairi Matatu aina Toyo, pamoja na hati zake ,mara baada ya kuibuka
mshindi kwa kuvuka malengo ya usambazaji wa vinywaji vya kampuni
hiyo. kulia ni Meneja wa Mauzo na Usamabazaji na TBL
Group Kanda ya Kusini ,James Bokella, wakati wa hafla iliyofanyia katika
kituo cha mauzo cha Ubungo .
Meneja wa Mauzo na Usambazaji na TBL Group Kanda ya Kusini
,James Bokella, (kushoto)akimwelekeza jinsi ya kuwasha pikipiki ya
matairi Matatu aina ya Toyo Meneja wa Kampuni ya Kibongoto ya jijini Dar e s
salaam, Nicetous Mtei ,mara baada ya kuibuka mshindi kwa kuvuka
malengo ya usambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi
wa kamapuni ya Rassam ya Banana Ukonga jijini Dar Es Salaam, Mwita
Magaiwa.
***************
Mawakala watatu wa kampuni ya TBL Group wanaofanyia
biashara zao jijini Dar es Salaam wamejishindia pikipiki za usambazaji
aina ya Toyo kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.9 baada ya
kuibuka washindi katika kampeni ya mauzo ambayo ilikuwa inaendeshwa na kampuni
kuanzia Mwezi Mei mwaka huu.
Hafla ya kukabidhi pikipiki hizo za kubebea mizigo imefanyika
katika kituo cha mauzo cha TBL Group cha Ubungo jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wateja na maofisa mbalimbali kutoka kampuni hiyo.
Akiongea wakati wa kukabidhi zawadi hizo,Mkuu wa kituo cha Mauzo na
Usambazi wa TBL kanda ya Kusini,James Bokella,alisema kuwa kampeni hiyo
iliyolenga kuwawezesha mawakala wadogo wa kampuni hiyo imefanyika kwa kipindi
cha miezi mitatu na kuwashirikisha wafanyabiashara 117 ambapo miongoni mwao
watatu wamevuka lengo la mauzo lililokuwa limewekwa na kampuni na wamefanikiwa
kujishindia pikipiki za kubeba mizigo aina ya Toyo.
Aliwataka wafanyabiashara hao kuwa ni Rasam Traders wa Ukonga,Kupata
Kuna Mungu Shop wa Mbagala na Kibongoto Investment wa Sinza “Wafanyabiashara
hao wamefanya vizuri katika kipindi cha kampeni ya kuvuka lengo la mauzo
ambalo kampuni ilipanga na leo wanakabidhiwa pikipiki za kubebea mizigo
kwa ajili ya kuwarahishia shughuli zao za biashara hususani usambazaji wa
vinywaji”.Alisema Bokella.
Aliongeza kuwa kampeni hii ni mwendelezo wa promosheni za kampuni
kupitia mpango wa kuwaendeleza wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa zake na
mbali na kuwapatia zawadi pia imekuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo
mbalimbali kwa ajili ya kukuza biashara zao ambapo wamekuwa wakipatiwa mafunzo
ya ujasiriamali,utunzaji wa vitabu vya fedha,matumizi mazuri ya fedha zao,usafi
katika maeneo yao ya biashara na kanuni na sharia za kufanya biashara nchini.
Alisema kampuni hiyo maarufu kama Retail Development Programme imepata
mafanikio makubwa kwa kuwafikia wafanyabiashara wengi wanaosambaza bidhaa za
kampuni na hivi sasa biashara zao zimeimarika zaidi na mitaji yao kuongezeka na
kuwafanya waishi maisha bora pamoja na familia zao.
Baadhi ya wafanyabiashara walioibuka washindi katika kampeni hii
wameishukuru kampuni ya TBL Group kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa
kuboresha maisha ya wateja wake “Ninayo furaha kujishindia pikipiki ya
kusambazia vijana,ushindi huu unadhihirisha kuwa tunafanya kazi na kampuni
inayotujali wateja wake”.Alisema mmoja wa washindi Mwita Magaiwa anayemiliki
biashara ya Rasam Traders.
Mshindi Mwingine Jackson Mushi mmiliki wa Kibongoto Investment amesema
kuwa inatia moyo kuona wawekezaji wakubwa kama TBL wanabuni mikakati ya kukuza
wafanyabiashara wadogo kama ambavyo wametoa pikipiki za kusambazia vinywaji
“Zawadi hii zinazidi kutupa motisha ya kufanya kazi kwa bidi”.Alisema
0 comments:
Post a Comment