RAIS wa Tanzania Dk
John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo
la Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Beatrice Shelukindo kilichotokea jana tarehe 02
Julai, 2016.
Beatrice
Shelukindo ambaye amewahi kuwa Mbunge Bunge la Afrika Mashariki na baadaye kuwa
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viwili mfurulizo
hadi alipostaafu mwaka jana 2015, amefariki dunia akiwa nyumbani kwao Njiro
Mkoani Arusha.
Katika salamu zake
Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo
hususani alipokuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwawakilisha
wananchi wa Jimbo la Kilindi na Mkoa wa Tanga.
“Beatrice
Shelukindo alikuwa kiongozi shupavu, ambaye siku zote alisimama kidete
kupigania maendeleo ya wananchi na kutetea rasimali za taifa.
“Kupitia kwako
Mhe. Spika Job Ndugai naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia,
ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu na pia kwa wabunge wote wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania” Amesema Rais Magufuli.
Dk John Pombe
Magufuli pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Beatrice Shelukindo
kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na
mpendwa wao na amemuombea marehemu apumzishwe mahali pema peponi, amina.
0 comments:
Post a Comment