Nafasi Ya Matangazo

July 10, 2016


 NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la Global Education Link katika manesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik Mollel akifafanua jambo.
 Naibu Waziri Jaffo (kushoto) akisindikizwa kundoka. BFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Wananchi waliotembelea banda hilo wakipata maelez ya huduma mbalimbali.
 ***********
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za elimu ni nyingi katika vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.

Jaffo ameyasema hayo wakati wa maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) katika banda la Global Education Link (GEL), amewataka Watanzania kutumia  maonyesho ya Sabasaba kuwa ni kipindi muafaka  kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo suala la elimu katika vyuo vya nje.

Jaffo amesema kuwa, maonesho ya sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa bure.

Aidha amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya nje ya nchi kwa gharama nafuu  watumie fursa hiyo kupita katika banda la Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.
‘’Serikali ya awamu ya tano ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli  imejipanga  hivyo kama wasaidizi wake lazima  tujipange kuhakikisha kwamba tuangalie jinsi ya  kubadilika kwa kasi na kubadilika huko kwa  kwa kasi lazima tuhakikishe tuna teknolojia yakutosha kabisa kwanza kiushindani, tuanzishe vitu ambavyo vitakuwa na soko kubwa”amesema .

Aliongeza kuwa  kuna fursa nyingi sio kwa serikali peke yake lakini hata kwa wazazi wenyewe kutumia fedha zao kwa mambo ya msingi kuliko kufanya  harusi  ya Sh. milioni 50 au milioni 100.

Amesema sh.milioni 50 zinazotumika katika harusi zinaweza kuziwekeza kwa vijana wetu katika kuwapatia elimu iliyo bora zaidi kwa ajili ya uchumi wa nchi yetu tunaweza kufanya vizuri zaidi.

Jaffo amesema kuwa udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ndani katika uhandisi, Udaktari wa Binadamu ni chache kutokana na mfumuko wa ufaulu kwa kidato cha sita pamoja na stashahada hivyo wanaweza kusoma katika vyuo vya nje ambavyo vimeweza kuwekeza katika maeneo hayo.

 “Leo hii nikwambie ndugu tembelea katika kila siku za mapumziko fanya  tathmini kila harusi iliyopo inayofanywa na sisi wenyewe ndio tunatengeneza harusi, unajikuta kumbe tungekuwa na mpango mkakati mzuri wa kuhakikisha jinsi gani vijana wetu tunakuwa na wataalamu katika sekta ya gesi, madini,  kilimo pamoja na  viwanda vidogo vidogo kwani kwa miaka mitano wenzetu kutoka nchi mbali mbali watakuja kutuchukua".amesema Jaffo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni yao hata baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya fedha anayetoa kwa kusomesha mtoto nje ya nchi.

Mollel amesema kuwa vyuo vya nje wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL ya kufatilia mienendo ya wanafunzi wao kwa kipindi chote wanachosoma  na taarifa zao zinatumwa na kisha mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.

 Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka  alisema kuwa GEL wanafanya kazi vizuri  katika kufanya utaratibu wa vijana kutafuta vyuo vya kusoma ambavyo vinatambulika na TCU.

Amesema kuwa wanaona jinsi gani ya kushirikiana na GEL na Chuo cha Mzumbe katika eneo la vyuo vya nje ili kuweza kufika sehemu nzuri kwa kubadilishana uzoefu.

Anita Ituwe ,amesema kuwa wakati alipokuwa anatafuta jinsi ya kupata vyuo vya nje walipata usumbufu lakini baada ya kufika GEL walipata maelezo ya kutosha na kuweza kujiunga katika chuo kimoja nchini India.

Nae Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Tanzania Taliki Abubakar ,amesema kwa wakati alipokuwa anatafuta chuo cha kusoma alikuwa hana uhakika lakini baada ya kukutana na GEL aliweza kupata Chuo cha kusoma na taratibu zilikwenda haraka.

Posted by MROKI On Sunday, July 10, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo