Nafasi Ya Matangazo

June 16, 2016

 MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akisaidia mafundi kuchanganya zege la kujengea kivuko cha Kiteputepu  wakati alipowatembelea wananchi wa kitongoji cha Kibundungulu kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe leo kuona adha wanayoipata wakati wa kuvuka katika kivuko chao.
 Eneo la kivuko cha Kiteputepu ambalo limebakia waya baada ya kivuko cha awali kusombwa na mafuriko. Serikali ya Mkoa imeahidi kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akisikiliza maelezo kutoka kwa wataalam juu ya ujenzi wa kivuko cha Kiteputepu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo amewatembelea wananchi wa kitongoji cha Kibundungulu kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe ambao tangu mwezi januari mwaka huu wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za jamii ikiwemo afya elimu na masoko kutokana na kukosa kivuko baada kivuko cha awali kusombwa na mafuriko.

Kutokana na kadhia hiyo kitengo cha maafa ofisi ya Waziri Mkuu ,tamisemi na ofisi ya Mkuu wa mkoa  kwa pamoja umewezesha mkandarasi kuanza kazi na kwa mujibu wa mkandarasi kazi hiyo itakamilika ndani ya wiki 2 na Mkuu wa Mkoa atakizindua kivuko hicho tarehe 8 julai mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi katika kipindi hiki kuacha kuvuka kwa kutumia waya zilizofungwa  kwasasa na  anaamini kujengwa kwa kivuko hiki kinawasaidia wananchi kuvuka hata kipindi cha mvua nyingi.

Hatua za kujenga kivuko hiki ni za dharura na muda mfupi na serikali itaweka katika mipango ili kujenga daraja la kudumu
Posted by MROKI On Thursday, June 16, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo