Mkurugenzi wa Mazingira wa SABMiller Africa,Muzi Chonko akifafanua jambo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari.
************
KAMPUNI ya kimataifa ya SABMiller inayomiliki viwanda vya kutengeneza
vinywaji sehemu mbalimbali duniani itaendelea kufanya biashara zenye mwelekeo
wa kubadilisha maisha ya jamii mbalimbali kuwa bora bila kusahau kuzingatia
utunzaji wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mazingira wa kampuni hiyo kanda ya
Afrika Bw.Muzi Chonco,alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
ambapo alipata wasaa wa kuelezea kanuni zinazoongoza utendaji wa kazi wa
kampuni kwa ajili ya kuleta mabadiliko endelevu sehemu zote ilikowekeza
duniani.
Chonco alisema kuwa tangu kampuni ianze kutumia kanuni hizo ambazo
zinashahabiana na malengo ya umoja wa mataifa tayari mafanikio mbalimbali
yameanza kupatikana na yapo matumaini ya kufikia mafanikio makubwa katika siku
za usoni.
“Tunapoongelea biashara endelevu tunamaanisha kuwawezesha wanachi kiuchumi kama ambavyo
tumekuwa tukifanya kazi na wakulima kupitia mpango wetu wa Go
Farming,kuwakwamua wanawake kiuchumi,kuendeleza wajasiriamali,kutunza vyanzo va
maji na kuwekeza katika miradi ya maji bila kusahau utunzaji wa mazingira”.Alisema
Chonco. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Alitoa mfano wa kampuni ya TBL Group ambayo iko chini ya kampuni hiyo kwa jinsi ilivyoweza
kufanya uwekezaji ambao umeleta mabadiliko nchini ambapo serikali na taaasisi
mbalimbali zinatambua mchango wake kwa kuitunukia tuzo mbalimbali ambazo
imekuwa ikishinda mwaka hadi mwaka.
Chonco alizichambua kanuni zinazoongoza kampuni na kuleta mabadiliko
kwenye jamii kuwa ni dunia
yenye nuru njema,dunia changamfu,dunia imara,dunia iliyo safi na dunia yenye nguvu kazi.
Alisema wakati umefika kwa wawekezaji mbalimbali kufanya uwekezaji
wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii badala ya kunufaisha upande mmoja “uwekezaji
unaoleta ajira za kila aina kwa wananchi,unaowawezesha kujipatia mapato kwa
kuuza bidhaa kwa kampuni iliyowekeza,kutunza mazingira na kuwapatia wananchi
elimu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vva maji,kusaidia makundi mbalimbali
kwenye jamii yaliyoachwa nyuma ukizingatiwa kwa vyovyote utaleta mabadiliko”.Alisisitiza.
Alitoa mfano kuwa ukimwezesha mkulima ataweza kupata kipato na kujenga
nyumba nzuri ya kuishi,watoto wake kusoma vizuri,familia yake kupata lishe bora
na kuongeza pato la familia kwa ujumla na maisha kubadilika kutoka hali duni
kuwa bora kama ambavyo imetokea kwa wakulima na makundi mengine
yanayoshirikiana na kampuni hiyo sehemu mbalimbali duniani.
0 comments:
Post a Comment